ASKARI KUTOKA VIKOSI MBALIMBALI VYA PEMBA WAFANIKIWA KUWAKAMATA RAIA SITA WA KENYA.

October 13, 2014
                           
                       NA MASANJA MABULA,PEMBA.
Kikosi kazi kinachojumuisha askari kutoka vikosi mbali mbali vya ulinzi Pemba wamefanikiwa kuwakamata Raia sita wa Kenya wakiendesha shughuli za  uvuvi katika eneo la bahari ya Kisiwa cha Zanzibar kinyume na utaratibu .

Wavuvi hao wakiwa na chombo chenye namba za usajili MV 066 V kikiwa na jina la Samira wamekamatwa siku ya Jumapili majira ya saa nane za mchana na askari hao wakiwa kwenye doria zao za kawaida katika eneo la Rasi Kiuyu .


Taarifa zaidi zinasema kuwa chombo hicho kimekuwa na kawaida ya kuja kuvua katika eneo la bahari ya Kisiwa cha Zanzibar kinyume na taratibu .


Akizungumza na mwandishi wa habari hizi , Mkuu wa Operation wa kikosi cha KMKM Pemba , Said Ali Ali amesema kuwa baada ya kufanyiwa upekuzi ndani ya chombo chao kulibaianika kuwepo mishipi 250 pamoja na boksi 5 za samaki .


Amesema kuwa chombo hicho kilikuwa kinaongozwa na nahodha wake Abdilah Kassim Ahmed ( 24) kikiwa pamoja na mahabaria watano ambao wote hawakuwa na paspoti na leseni za uvuvi .

 
Aidha amewatahadharisha wananchi kuwa askari wa kikosi kazi wako makini na wataendelea kuimarisha ulinzi wa mipaka ya nchi na kusisitiza mbali na kuzuia magendo ya karafuu pia kazi nyingine na kuhakikisha kwamba vitendo vyote vya hujuma ndani ya nchi havipewi nafasi .


Sheha wa Shehia ya Tumbe Magharibi Massoud Khamis aliwataka wananchi kushirikiana na vyombo vya ulinzi katika kutoa taarifa juu ya wageni wanaoingia hapa nchini ili kuweza kudhibiti kuitokea kwa maafa yanayoweza kuepukika .

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »