Waziriwa
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akiangalia
Jarida katika banda la Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
Idadi ya Watu Dunia (UNFPA – Tanzania) alipotembelea katika Maonyesho ya
Wiki ya Vijana leo mjini Tabora. Kutoka kushoto ni Mchambuzi wa Miradi
ya Vijana na Maendeleo wa UNFPA – Tanzania Bi. Tausi Hassan na Mshauri
wa Vijana wa Shirika hiloBw. John Kalimbwabo.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwezeshaji Vijana, Jinsia, Wanawake na Watoto
ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Bw. Ally Hamisa konyesha nyaraka za
vibali na sahihi za Wakuu wa Mikoa alipopita Kijana mzalendo Bw.Abiudi
Denis aliyetembea nchi nzima kwa Siku 65 kwa lengo la kuhamasisha
uzalendo ikiwemo kupinga Muundo wa Serikali Tatu, Kumpongeza Rais Jakaya
Kikwete na Kupinga watu wanaombeza Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius
Nyerere leo mjini Tabora wakati alipokea Bendera ya Taifa kutoka kwa
kijana huyo kwenye Viwanja vya Maonyesho ya Wiki ya Vijana. Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa
Elisante Ole Gabriel akitembelea mabanda wakati wa Maonesho ya Wiki ya
Vijana yanayoendelea katika Viwanja vya Ali Hassan Mwinyi mkoani
Tabora.
EmoticonEmoticon