Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe ikiwa ni ishara ya ufunguzi
rasmi wa jengo la hoteli ya Gold Crest linalomilikiwa na Mfuko wa
Pensheni wa PPF katika hafla fupi ya uzinduzi iliyofanyika hivi karibuni
jijini Mwanza.Wengine pichani toka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Mh.
Evarist Ndikilo,Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa PPF,ndg. Ramadhan
Kijjah,Naibu Waziri wa Fedha,Mh. Adam Malima,Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko
wa PPF,William Erio pamoja na Waziri wa Ujenzi,Mh. John Magufuli.
Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia katika hafla ya ufunguzi wa jengo
la kitega uchumi la hoteli linalomilikiwa na Mfuko wa PPF jijini Mwanza.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifatilia kwa makini maelezo ya Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa PPF Ndg. William Erio.
Naibu
Waziri wa Fedha,Mhe. Adam Malima (Mb) akihutubia wageni waalikwa katika
hafla ya ufunguzi wa jengo la kitega uchumi la hoteli inayomilikiwa na
Mfuko wa PPF jijini Mwanza. Ufunguzi huo uliambatana na Rais kutembelea
sehemu mbalimbali za jengo hilo la Hoteli.
Jengo la kitega uchumi la hoteli ya PPF Mwanza Gold Crest.
Mamia ya wakazi wa Mwanza wafurika katika hafla ya ufunguzi wa jengo la kitega uchumi la hoteli ya PPF Mwanza.
Mh.
Dkt Jakaya Mrisho Kikwete Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa
katika picha ya pamoja na baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya
Mfuko wa Pensheni wa PPF. Pamoja nao ni Waziri wa Ujenzi Mhe. John
Magufuli, Naibu wa Waziri wa Fedha Mhe. Adam Malima, na Mkuu wa Mkoa wa
Mwanza Mhe. Mhandisi Evarist Ndikilo.
Mh.
Dkt Jakaya Mrisho Kikwete Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa
katika picha ya pamoja na Menejimenti ya PPF mara baada ya kuzindua
jengo la kitega uchumi la hoteli ya PPF Mwanza.
Mh. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa PPF .
Mh.
Dkt Jakaya Mrisho Kikwete Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa
katika picha ya pamoja na Ndg. Meshack Bandawe Meneja wa PPF Kanda ya
Ziwa na Mratibu wa hafla ya ufunguzi wa jengo la kitega uchumi la hoteli
ya PPF Mwanza.
EmoticonEmoticon