WACHEZAJI watano wa timu ya Mgambo Shooting ya Tanga wanatarajiwa kuikosa mechi ya Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara dhidi ya timu hiyo na Kagera Sugar itakayochezwa kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani mkoani hapa.
Mchezo huo unatarajiwa kucheza Septemba 20 ikiwa ni ufunguzi wa pazia la michuano hiyo ambayo inashirikisha timu 14 kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini.
Kocha Mkuu wa timu hiyo Bakari shime alisema kuwa wachezaji hao wanakosa mechi hiyo kutokana na kuwepo kwenye timu za majeshi ambao ni Hassani Kibakuli, Salum Chambo, Full Maganga ambao huenda wasicheze mchezo huo wa ufunguzi wa ligi hiyo.
Alisema wachezaji wengine wawili wakiwemo beki wao wa kati Antony Chacha na Chande Magoja wapo kwenye kozi ya kijeshi hivyo wakimaliza wataungana na timu hiyo kwenye mechi zao za ligi kuu soka Tanzania bara.
Akizungumzia namna walivyojipanga kukabiliana na upungufu huo,Shime alisema kuwa wachezaji waliosalia kwenye kikosi hicho wana uwezo mkubwa katika nafasi hizo hivyo wana matumaini makubwa kucheza kwa mafanikio msimu ujao.
Alisema kuwa timu hiyo inaendelea vema na maandalizi ya kuelekea msimu mpya wa ligi kuu ambapo Ijumaa iliyopita walicheza na JKT Oljoro ya Arusha kwenye uwanja wa Sheirh Abeid Mkoani Arusha na kutoka suluhu pacha na Jumamosi walicheza na Panoni FC ya Kilimanjaro na kutoka Sare
ya 1-1.
Aidha alitoa wito kwa wadau wa soka mkoa wa Tanga kuzisapoti timu zao zilizopo mkoani hapa lengo likiwa kuhakikisha zinabaki kwenye michuano hiyo ili kuweza kukuza kiwango cha soka kwa kuzishabiki.
EmoticonEmoticon