Na Boniface Wambura, Dar es salaam
Kamati
ya Sheria na Hadhi za Wachezaji imepitisha usajili wa wachezaji wa
klabu za Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza huku wenye kasoro ndogondogo
klabu zao zikitakiwa kuziondoa ili waweze kupatia leseni za kucheza ligi
msimu huu wa 2014/2015.
Kasoro
hizo ni kufikia makubaliano na klabu ambazo wachezaji husika wametoka,
kuwafanyia uhamisho (transfer) na kulipa ada za uhamisho. Kamati
vilevile ilibaini wachezaji wengi hawakufanyiwa uhamisho kama kanuni za
ligi hizo zinavyoelekeza.
Hivyo,
klabu ambazo hazitakuwa zimeondoa kasoro hizo kwa wachezaji wao leseni
zao zitazuiliwa mpaka watakapokuwa wamekamilisha kila kitu. Ni wachezaji
wenye leseni tu ndiyo watakaoruhusiwa kucheza mechi za ligi.
Klabu
za African Lyon, African Sports, Ashanti United, Coastal Union, Kiluvya
United, Majimaji, Mji Mkuu, Polisi Dodoma, Polisi Morogoro, Red Coast
na Stand United ziliwawekea pingamizi wachezaji mbalimbali kwa
kutofanyiwa uhamisho.
Kuhusu
Ike Bright Obina wa Nigeria aliyewekewa pingamizi na African Lyon dhidi
ya Coastal Union, Kamati imezitaka klabu hizo kufikia makubaliano, na
zikishindwa mchezaji huyo atabaki African Lyon.
Kamati
vilevile ilijadili malalamiko ya Kocha wa zamani wa Simba, Zdravko
Logarusic dhidi ya klabu hiyo, na kuzipa pande hizo mbili siku 14
kufikia muafaka juu ya malalamiko hayo, na zikishindwa ndipo zirejee
tena mbele ya Kamati.
Logarusic
aliyewakilishwa na mwanasheria wake Dickson Sanga anailalamikia klabu
hiyo kwa kuvunja mkataba kinyume cha taratibu, hivyo kutaka Simba imlipe
dola 6,000 kwa kuvunja mkataba, na pia kulipa dola 50,000 ikiwa ni
fidia maalumu ya madhara yaliyotokana na uvunjwaji huo.
EmoticonEmoticon