Mkurugenzi
wa Kitengo cha Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO’s) wa Wizara ya
Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Bw. Marcel Katemba akiongea na
waandishi wa habari( Hawapo pichani)kuhusu juhudi zinazofanywa na
serikali katika kuyajengea mazingira mazuri ya ufanyaji kazi Mashirika
yasiyo ya Kiserikali (NGO’s) ili kuongeza ushiriki na kutoa mchango wao
katika kuleta maendeleo katika jamii,
Wakati wa Mkutano uliofanyika leo Jiijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano wa Wizara hiyo Bw. Erasto Ching’oro.PICHA NA GEORGINA MISAMA
***********************************
Na Jovina Bujulu-MAELEZO
Serikali
kupitia uratibu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto
imeendelea kujenga mazingira wezeshi kwa ajili ya Mashirika Yasiyo ya
Kiserikali (NGO’s) kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya ya jamii.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa usajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Marcel Katemba leo jijini Dar es Salaam.
Mercel
alisema kuwa serikali inaendeleza jitihada za kuwezesha Mashirika hayo
ikiwemo utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali
ya mwaka 2001 na Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na.24 ya mwaka
2002 na marekebisho yake ya mwaka 2005.
“Sera
hii ni mwongozo mkuu kwa Taifa katika masuala ya Mashirika Yasiyo ya
Kiserikali ikiwa na lengo la kuweka mazingira wezeshi kwa Mashirika hayo
kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya jamii kwa kuzingatia uwazi,
uwajibikaji na ushirikano” Alisema Marcel.
Marcel
aliongeza kuwa Bodi ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali
inaendelea kusimamia sekta ya mashirika hayo na kutoa ushauri kwa Waziri
mwenye dhamana ya uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ili
kuongeza ufanisi katika usimamizi wa sekta hiyo.
Aidha
Baraza la Taifa la NGO’s linaendelea kuratibu utekelezaji wa kanuni za
maadili ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kwa lengo la kujitawala,
kutandaa na kuboresha huduma zinazotolewa na mashirika hayo.
Akifafanua
zaidi Marcel amesema ubia na ushirikiano baina ya Serikali na NGO’s
umeimarika kutokana na matamko ya kisera na elimu inayotolewa kwa wadau
mbalimbali wa mashirika yasiyo yakiserikali.
Pia
Serikali imeendelea kutoa misamaha ya Kodi na ruzuku kwa Mashirika hayo
ikiwa ni sehemu ya kuthamini mchango wao katika maendeleo ya Taifa.
Juhudi
za serikali za kujenga mazingira wezeshi kwa NGO’s zimepanua wigo kwa
wananchi kujumuika na kushiriki katika maendeleo ya jamii ambapo zaidi
ya wananchi 35,000 ni wanachama wa mashirika hayo yaliyo zaidi ya 6679
kote nchini.
EmoticonEmoticon