KOCHA
Mkuu wa timu ya Mgambo Shooting ya Tanga, Bakari Shime amesema kikosi cha timu
hiyo kipo imara na kimekamilika vilivyo kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya
wa Ligi kuu soka Tanzania bara inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Septemba 20
mwaka huu hapa nchini.
Shime
alitoa kauli hiyo wakati akiongea na TANGA RAHA BLOG mara baada ya kumalizika mchezo wao maalumu wa kujaribu
matumizi ya mfumo wa kieletronici kati yao na African Sports ambapo timu hizo
ziitoka suluhu pacha ya kutokufungana, uliofanyika kwenye uwanja wa Mkwakwani
mkoani hapa.
Alisema
kuwa wao wataendelea na maandalizi ya kawaida kujiandaa na mechi yao ya Kagera
Sugar ikiwa ni kufungua pazia la michuano hiyo mikubwa hapa nchini na kuhaidia
kufanya vizuri kwa sababu ya kikosi hicho kuimarika kila siku.
Katika
hatua nyengine, Kocha Shime alisema uongozi wa timu hiyo umeingia mkataba wa
miezi sita na aliyekuwa mlinda Coastal Union, Said Lubawa kuichezea kwenye
msimu mpya wa Ligi kuu soka Tanzania bara.
Akizungumzia
sababu za wao kutokucheza mechi za majaribio,alisema kuwa mechi za aina hiyo
wakati mwengine zinaweza zikawa hazina faida kwa timu kutokana na kuwa timu
inaweza kucheza mechi hiyo lakini ikifika kwenye ligi kuu ikafanya vibaya.
EmoticonEmoticon