CHADEMA TANGA YASEMA KUWA ALIYEKUWA KATIBU WA WILAYA ALIYEJIUZULU HAKUWA KATIBU WAO

September 02, 2014
NA MWANDISHI WETU,TANGA.
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Tanga kimesema Khalid Rashid hakuwa katibu wake wa Wilaya ya Tanga kamaalivyoeleza wakati  akitangaza kujiunga na chama kipya cha ACT-Tanzania  bali alishafukuzwa kutokana na tuhuma za utovu wa nidhamu zilizokuwa zikimkabili.

Hali kadhailika wamesema kuwa majina  yaliyotangazwa na Khalid kujiuzulu pamoja naye wakidai ni wajumbe wa kamati ya utendaji hayakuwamo kwenye safu ya uongozi wa Chadema Wilaya ya Tanga bali ni ulaghai kwa wananchi na viongozi wa chama kipya alichoamua kujiunga.

Katibu wa Chadema Mkoa wa Tanga,Jonathan Bahweja  alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari wa kujibu taarifa ya katibu huyo na wajumbe wa kamati ya utendaji chadema waliyoitoa hivi karibuni.


Alisema kuwa Rashidi hakuwa tena mwanachama wala katibu wa Chadema Wilaya ya Tanga na hata hao aliowatangaza kwamba walikuwa wajumbe wa kamati ya utendaji majina yao hayamo kwa sababu nafasi zao zilianza kujazwa kutokana na kutokuwepo kwao.

Alisema Chadema mkoa imefurahishwa sana na hatua ya Khalid
kutangaza kujiunga na chama kingine kwa sababu katika kipindi cha miaka  zaidi ya 10 aliyokuwa akiongoza kabla ya kufukuzwa hakuweza kupata hata diwani mmja .

“Chadema Tanga wamefurahi sana alikuwa mzigo,fikiria katika kipindi chake cha uongozi kwa miaka zaidi ya 10,Chadema Tanga haina mbunge wala diwani anaondoka akiwa mtupu”alisema Bahweja

Katibu  huyo alisema hata hivyo Chadema haina muda wa kufanya
malumbano na mtu ambaye ameonyesha utovu wa nidhamu  bali kinajipanga kwa ajili ya kuhakikisha kuwa kinapata viti vingi kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa pamoja na wabunge na madiwani mwakani
.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »