N a Fadharkidev Blog
KOCHA wa Mtibwa Sugar Mecky Mexime,amesema kikosi chake
kimejiandaa kuitoa nishai Yanga katika mchezo wa ufunguzi utakaochezwa Septemba
20 kwenye uwanja wa Jamhuri Morogoro.
Mexime aliyewahi kufundishwa na kocha wa Yanga Mbrazili
Marcio Maximo wakati huo akiwa kocha wa ‘Taifa Stars,alisema namuheshimu kocha
huyo lakini hatokubali kuona timu yake ikipoteza mchezo huo wa ufunguzi tena
mbele ya mashabiki wao.
“Hatukuwa na matokeo mazuri sana msimu uliopita lakini
kwa sasa tumejipanga kuhakikisha tunarekebisha kasoro zutu ndiyo maana
tumefanya usajili mzuri ambao ninaimani tutapata matokeo ya ushindi kuanzia
mchezo wetu wa kwanza dhidi ya Yanga,”alisema Mexime.
Yanga ambayo itaanzia ugenini dhidi ya Wakata miwa hao wa
Manungu wanabidi kujipanga kwani hawana matokeo mazuri katika uwanja huo wa Jamuhuri
katika kipindi cha misimu mitatu iliyopita zaidi ya kuambulia kipigo na sare.
EmoticonEmoticon