Meneja Mauzo wa kampuni ya Megatrade Investment Ltd ya jijini Arusha ,Edmund Rutaraka(kushoto) akikabidhi msaada wa jezi kwa nahodha wa timu ya soka ya Machava fc. |
Meneja Mauzo wa kampuni ya Megatrade Investment Ltd ya jijini Arusha ,Edmund Rutaraka(kushoto) akikabidhi msaada wa jezi kwa mlinda Mlango wa timu ya soka ya Machava fc |
Meneja Mauzo wa kampuni ya Megatrade Investment Ltd ya jijini Arusha ,Edmund Rutaraka (kushoto)akikabidhi msaada wa jezi kwa Makamu mwenyekiti wa timu ya soka ya Machava fc,Abuu Masudi. |
MAGWIJI wa klabu ya Real Madrid ya Hispania leo (kesho) wanaendelea na ziara ya kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro ambapo kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na ofisi ya mkuu wa mkoa watatembelea lango la kupandia mlima Kilimanjaro la
Marangu.
Katika ziara hiyo ya kitalii chama cha soka mkoa wa Kilimanjaro (KRFA)
kimeiteua klabu ya soka inayoshiriki ligi daraja la kwanza ya Panone FC
kuwa wenyeji wa magwiji hao ambao pia watashuhudia mchezo wa
kirafiki kati ya timu za Panone fc na Machava fc utakaopigwa katika uwanja wa Ushirika.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama alisema ofisi yake imeandaa
utaratibu wa namna ya kuwapokea magwiji hao pamoja na kuandaa ratiba
maalumu ya kutembelea vivutio ukiwemo mlima Kilimanjaro pamoja na
kushuhudia mchezo mmoja wa Kirafiki.
“Katika tasnia ya michezo nchi yetu imepata bahati kubwa ya
kutembelewa na wachezaji wa zamani Real Madrid ambao pamoja na ziara
yao wamepanga kutembelea mkoa kwetu ,kikosi hicho kitaingia kati ya saa
tano au saa tano na nusu watashuka uwanja wa ndege wa KIA,”alisema
Gama.
Alisema baada ya kupokelewa moja kwa moja magwiji hao watapelekwa Mlima
Kilimanjaro katika ofisi za hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro KINAPA
ambako watapata fursa ya kupanda mlima huo kwa hatua chache baada ya
kupokea taarifa ya shughuli za utalii kwa ujumla.
“Tumewaandalia sehemu ya kupata chakula cha mchana na wenyeji wao klabu
ya Panone fc , baada ya chakula tukasema ni vizuri waone hatupo mbali
katika michezo, kwa hiyo tumepanga kuwa mchezo wa mpira wa miguu kati ya
Panone fc na Machava ikitanguliwa na ikitanguliwa na mechi ya vijana
chini ya miaka 15 .”alisema Gama.
Gama aliwataka wadau na wapenzi wa michezo mkoani humo kujitokeza na
kushiriki kikamilifu katika mapokezi makubwa ya wachezaji hao wa zamani
na kwamba licha ya kuwa dhamira yao ni kuimarisha utalii lakini pia
wangependa kuona hali ya michezo katika mkoa wa Kilimanjaro.
“Ni vizuri wakaona hali ya michezo katika mkoa wa Kilimanjaro na pengine
wakapata nafasi ya kuona vipaji vyetu ,mimi ninauhakika hapa kuna
wachezaji wanaweza kuchukuliwa na Real Madrid kwa sababu tunaweza
kufanya vizuri sana,,,kwa hiyo niwaombe wanamichezo wetu wajitokeze kwa
wingi tukawaone nyota hawa wa Madrid na pengine tuwape ukarimu wetu wa
kitanzania tuliouzoea.”alisema Gama.
Kwa upande wao klabu ya soka ya Panone fc kupitia msemaji wake Kassim
Mwinyi alisema wamefurahishwa na ujio huo na kwamba klabu imejipanga
kujenga mahusiano na magiwji hao kwa lengo la kubadilishana uzoefu
katika maswala ya michezo.
“Tumepata fursa kama Panone fc ya kukutana na Magwiji hawa wa Madrid
,sisi tumejipanga kutumia ujio huu katika kujenga mahusiano ya kitimu
kati yetu na wao ,na hakika utakuwa ni mwanzo mwema kwa klabu yetu
ambayo inajiandaa na ligi daraja la kwanza”alisema Mwinyi.
Magwiji hao watakao ongozwa na wanasoka waliowahi kutamba katika
ulimwengu wa soka kwenye ligi kuu ya Hispania maarufu kama La Liga,ligi
kuu ya Uingereza maarufu kama Bacrays,michuano ya Mabingwa na ile ya
kombe la dunia wakiwa na nchi zao wameanza kuwasili nchini kwa ajili ya
ziara maalumu.
Baadhi ya Wanandinga hao wa zamani waliotamba na Real Madrid kwenye
michuano ya La Liga, UEFA pamoja na kombe la dunia wakiwa na nchi zao
watakaofanya ziara ya siku nne nchini ni pamoja na Zinedine zidane, Luis
Figo, Fabio Cannavaro, Ronaldo De Lima, Christian karembeu na
Michael Owen.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya jamii Kanda ya kaskazini,
EmoticonEmoticon