Mechi kubwa: Manuel Pellegrini asema mechi dhidi ya Liverpool ni muhimu mno.
KOCHA
wa Manchester City, Manuel Pellegrini ameweka wazi kuwa kamwe hakuwahi
kuihofia Liverpool katika mbio za ubingwa msimu uliopita.
Kuelekea
katika mtanange wa jumatatu dhidi ya Liverpool katika dimba la Etihad,
Mchile huyo alisema kikosi cha Brendan Rodger kitakabiliwa na presha
kubwa mpaka kufikia mwezi mei mwaka huu.
Msimu
uliopita, Liverpool walipanda kileleni mwezi aprili mwaka huu baada ya
kuifunga City mabao 3-2 katika dimba la Anfield, lakini msimu
ulimalizika kwa machozi baada ya wakali hao wa Pellegrini kuwazidi kete
mwishoni na kutwaa ubingwa.
Katika msimu huo,makosa ya nahodha Steven
Gerrard yalichangia kufungwa na Chelsea wakiwa nyumbani na wiki moja
baadaye walitoka sare ya 3-3 na Crystal Palace katika dimba la Selhurst Park na kuzika matumaini ya ubingwa.
Mambo yalikuwa tofauti kwa City kwasababu walishinda mechi zote tano za mwisho na kuwapindua wakali hao wa Merseyside na kubeba 'ndoo'.
"Sikushangazwa,"
alikiri Pellegrini. "Nilikuwa na uhakika pale niliposema kwamba,
"Liverpool wanatakiwa kuwa makini kwasababu wanahitaji kucheza mechi nne
zaidi na presha ilizidi kuongezeka kila baada ya mechi wakiwa kileleni"
Jalamba: Manchester City wakijiandaa na mechi ya jumatatu uwanja wa Etihad dhidi ya Liverpool
Ataweza?" Frank Lampard amesema yuko tayari kucheza dhidi ya Liverpool
Pellegrini
anafikiria kuanza na Sergio Aguero aliyefunga bao katika mchezo wa
ufunguzi na kuwapa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Newcastle wikiendi
iliyopita.
Mshambuliaji
wa kimataifa wa Bosnian, Edin Dzeko anatarajia kuiongoza safu ya
ushambuliaji, lakini nyota mpya aliyesajiliwa kwa dau la paundi milioni
32, Eliaquim Mangala hayuko tayari kucheza baaada ya kujiunga na timu wiki iliyopita akitokea Porto
EmoticonEmoticon