Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akiwa mbele ya kaburi la Vedasto Kitwanga,mtoto wa
Naibu Waziri Nishati na Madini, Charles Kitwanga (Wanne kulia) wakati
alipokwenda nyumbani kwa Naibu Waziri huyo eneo la Usagara Mwanza
August 23, 2014 kumpa pole kufuatia kifo cha mwanae . Wengine pichani ni
mke wa Naibu Waziri huyo, Matrida (wanne kushoto) na kushoto kwa
Waziri Mkuu ni binti yao, Agness Misoji Kitwanga . Kulia ni Katibu wa
CCM wa Mkoa wa Mwanza, Joyce Masunga na Watatu kulia ni Mkuu wa Mkoa wa
Mwanza Mhandisi, Erasto Ndikilo.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Naibu Waziri wa Nishati na Madini,
Charles Kitwanga (kulia) baada ya kuwasili nyumbani kwa Naibu Waziri
huyo, eneo la Usagara, nje kidogo ya jiji la Mwanza ambako alikwenda
kumpa pole kufuatia kifo cha mwanae Vedastus Kitwanga kilichotokea hivi
karibuni. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akipigiwa magoti na Matrida Kitwanga (kulia) mke
wa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga (kulia) baada ya
kuwasili nyumbani kwa Naibu Waziri huyo, eneo la Usagara, nje kidogo ya
jiji la Mwanza ambako alikwenda kumpa pole kufuatia kifo cha mwanae
Vedastus Kitwanga kilichotokea hivi karibuni. Katikati ni binti wa
familia hiyo,Agnes Misoji Kitwanga.(Picha n Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na wadau wa ujenzi wa jengo lenye
Mnara wa kuongozea ndege katika uwanja wa ndege wa Mwanza unaoboreshwa
wakati alipofanya ziara ya kukagua maboresho ya uwanja huo August 23,
3024 Katikati ni Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dr. Charles Tizeba.(Picha na
Ofisi ya Waziri MKuu)
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akikagua eneo panapojengwa mnara wa kuongozea
ndege kwenye uwanja wa Mwanza August 23, 3014. Kushoto kwake ni Waziri
wa Uchukuzi, Dr. Charles Tizeba,(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na baadhi ya vibarua wanaofanyakazi
ya ujenzi wa jengo lenye Mnara wa kuongozea ndege katika uwanja wa ndege
wa Mwanza baada ya kukagua ujenzi huo August 23, 2014.(Picha na Ofisi
ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
vibarua wanaofanyakazi ya ujenzi wa jengo lenye Mnara wa kuongozea ndege
katika uwanja wa ndege wa Mwanza baada ya kukagua ujenzi huo August
23, 2014.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na vibarua wanaofanya
kazi ya kupanuzi wa uwanja wa ndege wa Mwanza wakati alipokagua upanuzi
wa uwanja huo August 23, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa
Pensheni wa Serikali za Mitaa (LAPF), Eliud Sanga (kulia) na Mkuu wa
Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Evarest Ndikilo baada ya kukagua ujenzi wa
jengo la Soko la Kimataifa linalojengwa kwa ubia kati ya jiji la Mwanza
na LAPF jijini humo August 23, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
EmoticonEmoticon