Rais Kikwete atawazwa kuwa chifu msaidizi wa waluguru na chifu kingalu huko kinole, morogoro, apewa jina la Chidukila

August 23, 2014


 CHIFU wa Waluguru Kingalu
Mwanabanzi wa 14, akijiandaa kumtawaza Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuwa Chifu Msaidizi wa kabila hilo katika sherehe za aina yake zilizofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi ya Kinole, kata ya Makuyuni, Morogoro vijijini Agosti 22, 2014.  Rais Kikwete pia alipewa jina la CHIDUKILA, lenye kumaanisha “muibukaji”, kwa maana ya kwamba Rais Kikwete ana uhuru wa kuibuka kijijini Kinole bila taarifa wala kusubiri kualikwa.
 CHIFU wa Waluguru Kingalu Mwanabanzi wa 14, akijiandaa kumvika mgolole Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa kumtawaza kuwa Chifu Msaidizi wa kabila hilo katika sherehe za aina yake zilizofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi ya Kinole, kata ya Makuyuni, Morogoro vijijini Agosti 22, 2014
 CHIFU wa Waluguru Kingalu Mwanabanzi wa 14, akimvika  mgolole Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa kumtawaza kuwa Chifu Msaidizi wa kabila hilo
 CHIFU wa Waluguru Kingalu Mwanabanzi wa 14, akimvipa pama lililosukwa kwa ukindu  Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa kumtawaza kuwa Chifu Msaidizi wa kabila hilo
 CHIFU wa Waluguru Kingalu Mwanabanzi wa 14, akimkabidhi kifimbo maalumu Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa kumtawaza kuwa Chifu Msaidizi wa kabila hilo
 CHIFU wa Waluguru Kingalu Mwanabanzi wa 14, akimuonesha  Rais Jakaya Mrisho Kikwete namna ya kuweka kifimbo maalumu begani wakati wa kumtawaza kuwa Chifu Msaidizi wa kabila hilo
 Mke wa Chifu Kingalu akimkabidhi Mama Salma Kikwete shuka katika sherehe hizo
 Chifu Msaidizi wa Waluguru Chidukila akifurahia wakati wa sherehe hizo
 Chifu Msaidizi wa Waluguru Chidukila akifurahia kifimbo maalumu alichokabidhiwa wakati wa sherehe hizo
 Chifu Msaidizi wa Waluguru Chidukila akiongea na wananchi wakati wa sherehe hizo
 Chifu Msaidizi wa Waluguru Chidukila akihutubia  wakati wa sherehe hizo
 Umati wa wananchi ukimsikiliza Chifu Msaidizi wa Waluguru Chidukila wakati wa sherehe hizo
 Hotuba ikiendelea 
 Chifu Msaidizi wa Waluguru Chidukila akisikiliza maelezo Mhandisi wa Maji wa Wilaya ya Morogoro Injinia Juliana J. Msaghaa akieleza juhudi za upatikanaji wa maji safi na salama wilayani humo wakati wa sherehe hizo
 Chifu Msaidizi wa Waluguru Chidukila  wakati wa sherehe hizo
  Chifu Msaidizi wa Waluguru Chidukila akifurahia pama lake wakati wa sherehe hizo
 CHIFU wa Waluguru Kingalu Mwanabanzi wa 14 akibadilishana mawazo na Rais Kikwete wakiwa na Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli (kulia), Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe Joel Bendera na kushoto ni msaidizi wa Chifu Kingalu
 Mama Salma Kikwete akihutubia wananchi wakati wa sherehe hizo, akisisitiza umuhimu wa kinamama kujiunga na SACCOS pamoja na kupambana na ugonjwa wa Fistula kwa wakati muafaka
Rais Kikwete akiwaaga wananchi wa Kinole baada ya sherehe hizo.
PICHA NA IKULU

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »