Kaimu
Mhifadhi wa Mbuga ya Ngorongoro, Bw. Amio Amio ambaye aliyemwakilisha
mgeni rasmi katika uzinduzi wa Mbio za Tigo Ngorongoro zilizofanyika
jana Aprili 19, 2014 kuanzia Mbuga ya Ngorongoro na kuishia mjini Karatu
akiongea machache wakati wa hafla ya kuwakabidhi washindi zawadi zao.
Pembeni yake ni Mkurugenzi wa Kanda wa Kampuni ya simu ya mkononi ya
TIGO, Brian Kalokola.
Kaimu
Mhifadhi wa Mbuga ya Ngorongoro, Bw. Amio Amio (kushoto) na Mkurugenzi
wa Kanda wa Kampuni ya simu ya mkononi ya TIGO, Brian Kalokola (kulia)
wakimkabidhi zawadi ya shilingi Mil. 1 mshindi wa kwanza wa Mbio za Tigo
Ngorongoro kwa kilomita 22 (Half Marathon) kwa upande wa wanaume,
Alphonce Felix mara baada ya kunyakua taji hilo kwa kuvunja rekodi kwa
kukimbia muda wa 1:03:59. Mbio hizo za Tigo Ngorongoro zilifanyika jana
Aprili 19, 2014 kwa kuanzia geti kuu la Mbuga ya Ngorongoro na kuishia
mjini Karatu. Tigo ndiyo walikuwa ni wadhamini wakuu wa mashindano hayo,
Mkurugenzi
wa Kanda wa Kampuni ya simu ya mkononi ya TIGO, Brian Kalokola (kulia)
akimkabidhi zawadi ya shilingi Mil. 1 mshindi wa kwanza wa Mbio za Tigo
Ngorongoro kwa kilomita 21 (Half Marathon) kwa upande wa wanawake,
Jackline Sakilu mara baada ya kunyakua taji hilo kwa kuvunja rekodi kwa
kukimbia muda wa 1:03:59.
Mwenyekiti mstaafu wa Chama Cha Riadha Tanzania, akitoa zawadi kwa Fabian Joseph aliyeshika nafasi ya nne,
Mwakilishi
wa kampuni ya Utalii ya ZARA ambao ndiyo waandaaji wa mashindano hayo
akitoa zawadi kwa mshindi wa saba kwa upande wa wanawake.
Washindi
wa Mbio za Tigo Ngorongoro upande wa wanawake wakiwa wamejipanga
kusubiri zawadi zawadi zao… kutoka kulia mshindi wa kwanza Jackline
Sakilu, Nathalina Elisante, Marry Naali, Failuna Abdi na Flora Yuda.
Wanariadha
wa Mbio za Tigo Ngorongoro Kilometa 21 (Half Marathon) wakianza mbio
katika geti kuu la Mbuga ya Ngorongoro na kuishia mjini Karatu.
Mchuano wa wanariadha ukiendelea kwa kasi.
Ilikuwa ni patashika nguo kuchanika kila mmoja akitaka kuchomoza ili aweze kushinda.
Mshindi
wa kwanza wa Mbio za Tigo Ngorongoro kilomita 21 (Half Marathon) kwa
upande wa wanaume, Alphonce Felix akiwachomoka wenzake.
Mshindi
wa kwanza wa Mbio za Tigo Ngorongoro kwa kilomita 21 (Half Marathon) kwa
upande wa wanaume, Alphonce Felix akimaliza kwa furaha.
Mshindi
wa kwanza wa Mbio za Tigo Ngorongoro kwa kilomita 21 (Half Marathon) kwa
upande wa wanawake, Jackline Sakilu akimaliza mbio.
Umati wa Wakazi wa Mji wa Karatu wakifuatilia michuano hiyo.
Hapa ndipo kulipoanzia kwa mbio za makampuni... ambapo makampuni yalikimbia kilometa 5.
Mshindi wa kwanza wa mbio za makampuni akifurahia mara baada ya kumaliza.
Mkururenzi Mtendaji wa Kampuni ya Frontline Porter Novelli, Irene Kiwia hakuwa nyuma kushiriki mbio hizo.
Washiriki wa Mbio za Tigo Ngorongoro Kilometa 5 za Makapuni wakimenyana vikali.
Timu ya
Kampuni ya Frontline Porter Novelli ya jijini Dar es Salaam wakiwa
katika sura ya furaha mara baada ya kumaliza kukimbia Kilometa 5 katika
Mbio za Tigo Ngorongoro.Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason
Blog..
EmoticonEmoticon