MZEE WA MIAKA 61 AKATWA SEHEMU ZAKE ZA SIRI ILEJE MBEYA

April 21, 2014

Gari ya wagonjwa toka Ileje ikiingia Hospitali ya rufaq Mbeya  
Majirani wakimuhudumia majeruhi
NA Ezekiel Kamanga,Ileje Mbeya- Mbeya Yetu Blog.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la London Haonga(61) mkazi wa Kijiji cha Mapogolo Kata ya Mbebe Wilaya ya Ileje Mkoani Mbeya amejeruhiwa vibaya kwa kukatwa nyeti zake na watu watatu wasiofahamika kisha kutokomea nazo kusikojulikana.

Tukio hilo limetokea majira ya saa mbili usiku April 19 mwaka huu baada ya mmoja kati ya watuhmiwa kufika nyumbani kwa mzee huyo kisha kubisha mlango akiomba msaada wa kuonyeshwa njia akidai amepotea njia.

Mzee London alipotoka nje ya nyumba akiwa anamwelekeza njia mtu huyo anayedaiwa kuwani mjukukuu wake mita chache kutoka nyumbani kwake alifunikwa na kitambaa usoni na watu wawili kisha kuangushwa na kukatwa nyeti zake ambazo waliondoka nazo.

Mtendaji wa Kijiji cha Mapogolo Cosmas Haonga amesema baada ya unyama huo Mzee London alipoteza fahamu na alipozinduka alipiga yowe kuomba msaada ambapo majirani walifika na kutoa msaada wa kumkimbiza Hospitali ya Wilaya ya Ileje huku wakiwasaka watuhumiwa wa tukio hilo.

Kwa mujibu wa Mtendaji wa Kijiji imedaiwa kuwa watuhumiwa wa tukio hilo wanatokea Mpemba wilaya ya Momba ambao walitambuliwa na mhanga wa tukio hilo ambapo baada ya kupewa PF 3 mzee London amekimbizwa Hospitali ya Rufaa Mbeya ambapo alifikishwa Hospitali ya Rufaa majira ya saa 11:00 jioni April 20 huku akilalamika kwa maumivu makali.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ahmed Msangi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kudai kuwa chanzo cha awali imedaiwa sababu za kutendewa ukatili huo umetokana na mmoja wa ndugu aliyedai kuwa mzee huyo anatuhumiwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mke wa mdogo wake hivyo watu hao walitumwa kwa nia ya kulipiza kisasi.

Aidha imedaiwa kuwa baadhi ya viungo vimekamatwa na wengine kudai kuwa tukio hilo kuhusishwa na imani za kishirikina kwani imedaiwa watuhumiwa kuimbilia nchi jirani mara baada ya kutenda kitendo hicho cha kikatili.

Kamanda Msangi ameoa wito kwa jamii kuacha tabia za kujichukulia sheria mkononi amesema pindi wanapokuwa na migogoro ni vema kutatua migogoro kwa njia ya mazungumzo ili kuleta amani na kuahidi wale wote waliohusika na tukio hili wanakamatwa na kufikishwa kwenye mikono ya sheria kwani hakuna mtu aliye juu ya sheria.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »