Wanariadha
wa Mbio za Ngorongoro Marathon, Kilometa 21 (Half Marathon) wakianza
mbio katika geti kuu la Mbuga ya Ngorongoro na kuishia mjini Karatu.
Mchuano wa wanariadha ukiendelea kwa kasi.
Ilikuwa ni patashika nguo kuchanika kila mmoja akitaka kuchomoza ili aweze kushinda.
Mshindi
wa kwanza wa Mbio za Ngorongoro Marathon kilomita 21 (Half Marathon)
kwa upande wa wanaume, Alphonce Felix akiwatoka wenzake.
Mshindi
wa kwanza wa Mbio za Ngorongoro Marathon kwa kilomita 21 (Half
Marathon) kwa upande wa wanawake, Jackline Sakilu akimaliza mbio.
Umati wa Wakazi wa Mji wa Karatu wakifuatilia michuano hiyo.
Hapa ndipo zilipoanzia mbio za makampuni... ambapo makampuni yalikimbia kilometa 5.
Mkururenzi Mtendaji wa Kampuni ya Frontline Porter Novelli, Irene Kiwia (nyuma) hakuwa nyuma kushiriki mbio hizo.
Washiriki wa Mbio za Tigo Ngorongoro Kilometa 5 za Makapuni wakimenyana vikali.
Timu
ya Kampuni ya Frontline Porter Novelli ya jijini Dar es Salaam wakiwa
katika sura ya furaha mara baada ya kumaliza kukimbia Kilometa 5 katika
Mbio hizo.
EmoticonEmoticon