ASKOFU WA JIMBO KATOLIKI LA NJOMBE AWATAKA WABUNGE WA BUNGE LA KATIBA KUWA NA HOFU YA MUNGU

April 21, 2014
Na Prosper  Mfugale, Njombe
Askofu Wa Jimbo Katholiki La Njombe Alfred Maluma Amewataka Wajumbe Wa Bunge Maalumlu La Katiba Kutangulizi Hofu Ya Mungu Katika Kuijadili Na Kuichambua Rasimu Ya Katiba Mpya Ili Taifa Liweze Kupata Katiba Bora Itakayowafaa Watanzania.
Ameyasema Hayo Kwenye Misa Ya Mkesha Wa Pasaka  Katika Kanisa  Katoliki Jimbo La Njombe Wakati Akihubiri Injili Maalumu Ya Mkesha Huo.
Askofu Maluma Amesema Takribani Miaka Hamsini Ya Uhuru Taifa La Tanzania Limekuwa Likipokea Wageni Mbalimbali  Kufuatia Hali Ya Amani Ambayo Imetokana Na Muungano Imara Ulioanzishwa Na Waasisi Wa Taifa Hilo
Amesema Watanzania Hawana Budi Kuendelea Kuliombea Bunge Maalumu La Katiba Ili   Katiba Bora Ipatikanae Ambayo Italeta Haki Na Demokrasia Kwa Watanzania Wote Nasio Wachache.
 Pia Ametumia Fursa Hiyo Ya Mkesha Kumshukuru Raisi Wa Jamhuri Ya Muungano Kwa Kuamua Kuwaruhusu Watanzania Kuunda Katiba Mpya Ya Kisheria Ambayo Itatea Haki Na Demokraia Kwa Wote

Katika Hatua Nyingine Amesema Anashangazwa Na Kitendo Cha Baadhi Ya Wajumbe Wa Bunge Maalumu Wa Bunge La Katiba Kutumia Bunge Hilo Kwa Kufanya Mizaha Badala Ya Kujadili Rasimu Kama Walivo Tumwa Kuwawakilisha Watazania Waliobaki Na Kuongeza Kuwa Iwapo Muungano Utavunjika Heshima Ya Taifa Hilo Haitakuwepo Na Kwamba Taifa Hilo Halita Tawalika Kama Ilivyo Sasa

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »