MMH..CHADEMA...TAALUMA SI KIGEZO KIKUBWA CHA KUPATA UBUNGE...JE NI SAHIHI?!

April 21, 2014

1) Godbless Jonathan Lema -- Diploma
2) Antony Gervase Mbassa - - Adv diploma - KCMC
3) Prof Kulikoyela Kanalwanda Kahigi --- Phd
 4) Freeman Aikaeli Mbowe – Form six

5) Highness Samsoni Kiwia ---- Secondary education – O level  
6) Simon Peter Msigwa - -- O level,  
7) Yohana Israel Natse --- Diploma in Education,
8) Halima James Mdee --- Degree, UDSM  
9) Zitto Zuberi Kabwe --- Degree (economic) UDSM, Masters degree (MLB)  
10) Silvester Mhoja Kasulumbay – Primary,  
11) John Magale Shibuda --- O LEVEL  
12) Joseph Osmund Mbilinyi --- Form IV  
13) David Ernest Silinde --- Degree(BCOM), UDSM  
14) Mustapha Boay Akunaay – Degree in law, Open University  
15) Meshack Jeremiah Opulukwa --- Not updated  
16) Philemon Ndesamburo --- Advanced diploma in Shipping  
17) Said Amour Afri --- Primary school  
18) Vicent Kiboko Nyerere -- O level  
19) Ezekia Dibogo Wenje --- Degree, St Augustine  
20) Joseph Roman Selasini --- Degree, UDSM  
21) Tundu Antiphas Mughwai Lissu ___ LLM – Masters degree  
22) John John Mnyika --- CV not updated  
23) Salvatory Naluyaga Machemuli ___ Degree – DIT  
24) Joshua Samwel Nassari – Not updated
Msitari mwekundu kwa Uongozi wa juu nchini kama Ubunge unatakiwa uwe juu ya Advance diploma, Hili la Ubunge kwa chadema ni kama vile Mheshimiwa slaa alivyotangaza Kirahisi kuhalalisha gongo kwa lengo la kuvuna kura za wanywa gongo eti atakuza uchumi kupitia watengeneza gongo na wanywaji! Kasahau kwamba gongo hata kama sio sumu ila inaweza kutengeneza genge la wavivu kufanya kazi, Hawajali taaluma na wanazidi kujitetea na kutangaza kwamba elimu sio kigezo cha lazima kwenye uongozi kwani wasomi wa ccm wamechemsha tangu Uhuru!. 
Ukweli ni kwamba ukiondoa wabunge wasomi wachache wa chadema wengine ni wapiga kelele tu Bungeni wanafanya kuonekana tu kwamba wanaongea lakini ni wabunge wasio na mtazamo wambali wanaona mwisho wa pua zao tu. 
Taifa zima linapaswa kuamua sasa Kukataa kuongozwa na waigizaji wa Darasa la saba, na lazima tusitumie maneno rahisi kujenga jamii isiyothamini elimu Kama tunavyoaminishwa na wanasiasa rahisi hawa ambao kwasasa wanaonekana kivutio kwa wasiosoma kama akina afande sere, JB, Ray, Mzeemajuto ambao lengo lao kusaka ubunge nikuongeza umaarufu wao ila hawana vission yeyote kwa Watanzania. 
Bungeni sio sehemu ya kuenda kufanya sanaa, Bungeni sio kwenda Kuchekesha Bali nikuenda kuwawakilisha watu milioni karibia hamsini sasa ambao asilimia 80 wanaishi katika umasikini wakutupwa, acha mwanamziki afanye kazi ya mziki, muigizaji aigize, mchekeshaji achekeshe nasio kukimbilia mambo mazito ya kitaifa kwa umaarufu rahisi walionao. 
Tujiulize swali Tunajenga Taifa gani kwa kuongoza na Darasa la 7 au wasanii?  Hivi mzee majuto anataka aende Bungeni Kufanya nini kama sio dharau kwa Bunge letu?  Mtu kama Lema au Sugu Ufahamu wake unaweza kulitoa taifa letu toka katika umasikini? au ndio tunazidi kuongeza migogoro katika jamii?  
Tusitumie Kigezo rahisi Eti wasomi wameshindwa basi kilamtu awe kiongozi katika jamii, angalia ukweli Hivi mtu kama zitto au J Mnyika anaposimama bungeni unaweza kufananisha na sugu au Lema. 
Taifa lolote lililoanza kupoteza Muelekeo linaanza kukumbatia wasio soma na wahuni kama akina lema na sugu na hii ni dalili mbaya Lazima Tujitambue na Tutambue athari za mfumo huu unaojongea Taratibu, Tusipokuwa makini Tutafanya kosakubwa sana kwa kuongozwa na Dicteta ambae kichwa chake ni sifuri kabisa. 
Chadema Kama chama Mbadala talajali wa CCM, jitahidini kutujengea viongozi Bora, shawishini wasomi wagombee nafasi kubwa kama ubunge na msiangalie umaarufu wa mtu kwasababu baadaye mkipewa nchi mawaziri watabaki kunywa gongo, kuvuta bangi, kufanya maigizo, na kuimba bongo flever tu badala yakuwa serious kujenga Uchumi. 
Wabunge ambao ni darasa la saba je wanajiendeleza kielimu au ndio wamebweteka wakijua chadema Hakuhitaji wasomi? au nadharia yenu ya kuogopa umaarufu wao ndio bado itawapa nafasi ya kugombea ubunge tena 2015?, Tuleteeni akina Mnyika, akina mdee, akina zitto wengi2015 nasio kutujazia watu waliokimbia umande eti wanaweza kwakuwa wapiga kelele wasiojua hata uelekeo. Uchaguzi wa 2015 lazima Uwe uchaguzi utakaotuletea wasomi vijana wengi bungeni, Sugu, Lema, Majimarefu, Murugo, wote jiandaeni kugombea labda udiwani na hata baadhi yenu udiwani pia hauwafai gombeeni serikali za mtaa mwakani.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »