HATIMAE MSEMAJI WA P-SQUARE AONGEA KUHUSU TETESI ZA KUVUNJIKA KWA KUNDI

April 21, 2014

Wiki hii mitandao ya Nigeria iliripoti kuwa kulikuwa na ugomvi mkubwa kati ya mapacha wanaounda kundi la PSquare, Peter na Paul Okoye na kwamba walitaka kupigana wakati wakiwa mazoezini.

Habari hizo zilichochewa na tweet ya kaka yao mkubwa ambaye ni meneja wao, Jude Okoye iliyootafsiriwa na mitandao hiyo kuwa huenda ameachana na kundi hilo baada ya kuwepo ugomvi kati yake na ndugu hao kutokana na msimamo wake wa kutohudhuria ndoa ya kisasa ya mdogo wake itakayofanyika Dubai.

Mitandao hiyo iliandika kuwa Jude Okoye hapatani kabisa na mke wa Peter Okoye, Lola Omotayo.

“After over 10 years of hard work, it’s over. Am done.” Alitweet Jude Okoye.

Hata hivyo, msemaji wa kundi hilo anaejulikana kama Bayo Adetu amekanusha habari hizo wakati akiongea na Premium Times na kudai kuwa hafahamu habari hizo zimetoka wapi.

“I am too busy to give some wanna be blogger traffic, I don’t know where that report is coming from. Maybe they just want to get traffic to their site. It’s baseless and untrue.” Amesema Bayo Adetu.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »