April 01, 2014

SSRA YATOA TAARIFA KUHUSU UANDIKISHWAJI WANACHAMA KATIKA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII NCHINI

Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA),Ansgar Mushi (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu uandikishwaji wa wanachama wapya wa mifuko ya Hifadhi ya Jamii nchini. Kulia ni Mkurugenzi wa Sheria wa SSRA, Ibrahim Ngabo.      

Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA),Ansgar Mushi (wa pili kushoto), akisoma taarifa hiyo kwa waandishi wa habari. Kutoka kulia ni Ofisa Habari wa SSRA, Mr Stewart,Mkurugenzi wa Idara ya Fedha na Utawala, Mohamed Nyasamo, Mkurugenzi wa Sheria  , Ibrahim Ngabo na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Uhamasaishaji, Sarah Kibonde.
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA),Ansgar Mushi (kushoto), akisisitiza jambo katika mkutano huo.
 Wanahabari waliokuwepo kwenye mkutano huo wakichukua taarifa hiyo. (Imeandaliwa na www.mwaibale.blogspot.com)
Mkurugenzi wa Sheria wa SSRA, Ibrahim Ngabo (kulia), akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu masuala mbalimbali ya kisheria.
Na Dotto Mwaibale

MAMLAKA ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) imesema haitasita kumchukulia hatua mtu yeyote anayekiuka sheria za kujiunga na mfuko wowote ulioanzishwa kwa sheria ya Bunge.

Hayo yalibainishwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Ansgar Mushi wakati akitoa taarifa kwa umma kupitia kwa waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu uandikishwaji wa wanachama wapya wa mifuko ya Hifadhi ya Jamii nchini.

Alisema SSRA jukumu lake kubwa ni kusimamia na kudhibiti shughuli zote za sekta ya Hifadhi ya Jamii nchini ikiwa ni pamoja na Mifuko yote ya Hifadhi ya Jamii iliyoanzishwa kwa sheria za Bunge ambayo ni NSSF, PSPF,PPF,GEPFE, LAPF na NHIF.

"Kwa mamlaka tuliyonayo hatutasita kumchulia hatua mtu yeyote atakayekiuka sheria zilizopo za uandikishaji wa wanachama wapya katika mifuko hiyo baada ya kuwepo kwa ukiukaji huo" alisema Mushi.

Alisema sheria inayoruhusu mifuko hiyo kuandikisha wanachama wapya wanaoingia kwa mara ya kwanza kwenye ajira kutoka sekta rasmi au sekta binafsi isikiukwe.

Alisema sheria hiyo namba 5 ya mwaka 2012 pia inaruhusu wafanyakazi ambao wako kwenye ajira lakini hawajawahi kuandikishwa na mfuko wowote kujiunga na mfuko watakaouchagua.

Mushi alisema kuwa siku za hivi karibuni kumeibuka malalamiko ya uandikishaji wa wanachama wapya na kuwa baadhi ya vitendo vinavyolalamikiwa ni mfuko kutengeneza, kutoa nyaraka za uwongo kwa madhumuni ya kupotosha umma na hali halisi ya kupata ridhaa ya wafanyakazi,waajiri na wadau wengine.

Alitaja mambo mengine kuwa ni kuandikisha wafanyakazi kwenye mfuko kwa lazima wakati yupo kwenye mfuko mwingine na mwajiri kumlazimisha mfanyakazi kujiunga na mfuko fulani.

Mushi alitaja malalamiko mengine kuwa ni mwajiri kuwa na sera au miongozo ya ajira inayoelekeza wafanyakazi wake kujiunga na mfuko fulani na matumizi ya njia za usajili zisizifaa kuandikisha wanachama.

Alisema vitendo hivyo vyote vimeharamishwa chini ya Sheria namba 8 ya mwaka 2008 na miongozo ya uandikishaji wanachama (socia Security Schemes (Memberrship Registration) Guidelines,2013 iliyotolewa chini ya sheria hiyo na kuwa yeyote atayejihusisha na vitendo hivyo anavunja sheria.

Mushi alisema SSRA inapenda kuwakumbusha ,Mifuko yote ya Hifadhi ya Jamii pamoja na wadau wote wakiwemo waajiri na wafanyakazi kuzingatia matakwa ya Sheria namba 8 ya mwaka 2008 pamoja na miongozo ya uandikishaji wanachama ili kulinda uhuru wa wanachama wa kujiunga na Mfuko wanaoupenda.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »