SERIKALI ITAHAMISHA NA KUWONDOKA WANANCHI WAISHIO KANDO KANDO YA BONDE LA MTO MKOMAZI-JK
NA OSCAR ASSENGA,KOROGWE
SERIKALI
imesema itahamisha makaburi na itawaondoa wananchi wote wanaoishi kando
kando ya bonde la mto mkomazi kwa kuwalipa fidia za makazi na mimea yao ili kupisha
ujenzi wa bwawa kwa ajili kuinua na kuendeleza kilimo
cha umwagiliaji.
Rai
hiyo ilitolewa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dokta Jakaya Mrisho
Kikwete wakati akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara
uliofanyika katika viwanja vya mamlaka ya mji wa mombo wakati wa ziara yake ya
kukagua shughuli za maendeleo ya wananchi wilayani korogwe.
Rais
Kikwete aliyasema hayo mara baada ya mkurugenzi
mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Korogwe Lucas Mweri kueleza kwamba
serikali ilishatoa kiasi cha shilingi milioni 800 ili kutengeneza mradi huo
lakini wananchi walikataa kuondoka katika maeneo hayo kwa madai kwamba ni
maeneo yao ya siku nyingi kwa shughuli za kilimo, mifugo, makazi lakini
pia katika maeneo hayo yapo makaburi ya ndugu zao.
Rais
kikwete aliwaeleza wananchi kuwa hakuna mwananchi mwenye
ardhi , Ardhi ni ya serikali na kwamba mwenye mamlaka ya mwisho katika
ardhi ni Rais hivyo amesema wananchi hao wataondolewa katika maeneo hayo kwa
hali yoyote na gharama yoyote na kwamba hakuna kaburi lolote litakalo tumbukia
katika bwawa hilo.
Kikwete
alisema makaburi yote yatatafutiwa maeneo maalum kwa
kuhamishwa mabaki ya miili na kuzikwa upya kwa imani za kidini za
ndugu zao.
Hata
hivyo alisema serikali inapotaka kufanya jambo lolote la maendeleo hakuna
kikwazo kitakachowekwa na mwananchi yeyote, na kwamba ni lazima serikali
iendelee kuelekeza nguvu zake katika kilimo ili wananchi waweze kujikwamua na
umaskini.
EmoticonEmoticon