BANZASTONE KUTAMBULISHWA JANUARI 25
MTUNZI na mwimbaji wa bendi ya Extra Bongo 'Next
Level Wazee wa Kizigo' Ramadhani Masanja 'Le General Banza Stone' anatarajiwa
kutambulishwa rasmi kurejea kwake upya jukwaan Januari 25 mwaka huu katika
onyesho maalumu litakalofanyika katika Ukumbi wa Meeda Club Cnza jijini Dar es
Salaam.
Kwa muda wa miezi miwili Banza alikuwa yu mgonjwa
hali iliyomsababishwa kushindwa kupanda jukwaani kabla ya hivi karibuni kujikongoja
na kushiriki kwenye ziara ya 'Mafahari Watatu' katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa
akiwa na Extra Bongo.
Kwa mujibu wa msemaji wa bendi hiyo Juma Kasesa,
mara baada ya kumalizika kwa ziara hiyo Banza amepewa mapumziko maalumu ya wiki
tatu kuimarisha afya yake na kufanya mazoezi tayari kujiandaa kurejea jukwaani
kwa kishindo kuwapa burudani wapenzi na mashabiki wa muziki wa dansi waliokuwa
waki -mis sauti na tungo zake.
“Tumeamua kumpa wiki tatu apumzike ambapo
atazingatia kula vizuri, mazoezi binafsi sambamba na kupata muda wa kupumzika ili
aweze kurudisha afya awe katika muonekano tofauti na sasa,” alisema.
Katika ziara ya Kanda ya Ziwa Banza alipata nafasi
ya kuweza kuimba vipande vyake (mega mix) ingawa hakuweza kupewa nafasi ya
kukaa muda mrefu stejini kutokana na afya kutoimarika vya kutosha.
Alisema, Extra Bongo kwa kutambua thamani ya afya ya mwanamuziki wake imeamua kumpumzisha Banza ili kujipanga kuwapa ujio wake mpya aliowaandalia wadau wa muziki wa dansi.