BAADA YA KUZUSHIWA KIFO MWAKA JANA D.DOCTOR AKANUSHA HABARI HIZO.

January 10, 2014

MSANII D.DOCTOR AKIWA KATIKA POZI LEO
                       Na Oscar Assenga,Tanga.
MSANII nguli wa mziki wa Bongofleva mkoani Tanga, Dominick Mndeme “D.Doctor amejitokeza hadharani na kukanusha habari zilizokuwa zimeenezwa kuwa amefariki dunia kwa kusema sio kweli.

Akipiga stori na  TANGA RAHA BLOG,D.Doctor alihabarisha kuwa habari hizo zilivumishwa Desemba 29 mwaka jana na mmoja kati ya wasanii nguli wa jijini Tanga ambaye ni rafiki yake wa karibu kitendo ambacho kilimshangaza sana.


  “Mimi sijafa ni mtu tu alichukua simu yangu bila mimi kujua akaanza kueneza habari kuwa mimi nimekufa na aliweza kufanya hivyio baada ya mimi kuzidiwa kilevi na kuzima ghafa ndio jamaa huyo nisiyemjua ndipo alipoamua kueneza habari hizo hali ambayo iliwafanya marafiki na ndugu zangu kushtuka sana na kudhani habari hizo ni za kweli “Alisema D.Doctor.
MSANII WA MZIKI WA BONGOFLEVA MKOANI TANGA,DOMINICK MNDEME "D.DOCTOR"AKIWA KATIKA PICHA
 Alisema baada ya kutokea hali hiyo aliweza kupokea simu  kutoka nchi mbalimbali ambao walikuwa na lengo la kuthibitisha habari hizo ambao walikuja kubaini kuwa habari hizo hazina ukweli wowote.

Aidha aliwaomba radhi mashabiki wake,ndugu na marafiki zake kwa usumbufu wowote ambao ulijitokeza na kuwataka mashabiki wake watarajie kupata ngoma kali ambazo zinakuja hivi karibuni.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »