D.DOCTOR :AWASAA WASANII KUWA WABUNIFU.

January 10, 2014
Na Oscar Assenga,Tanga.
WASANII wa mziki wa BongoFleva nchini wametakiwa kuwa wabunifu na kubadilika kutokana na mazingira ili kuendana na kasi ya maendeleo na kuutangaza mziki huo kitaifa na kimataifa kama ilivyokuwa kwa nchini nyengine duniani.

Wito huo ulitolewa na Msanii wa mziki huo mkoani Tanga,Dominick Mndeme “D.Doctor wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi ambapo alisema kutokuwa na umakini kwa wasanii wengi  kumewafanya kutoka na kuonekana kuwika kwa muda fulani na baadae kupotea kwenye tasnia hiyo kitendo ambacho kinachangia pia kushusha mziki huo.


Alisema licha ya kuwa mziki huo kupiga hatua kubwa sana hapa nchini zipo changamoto mbalimbali ambazo zinawakabili ikiwemo kubaguliwa na baadhi ya vyombo vya habari kuchezwa nyimbo zao kutokana na uchanga walionao kwenye tansia hiyo.

    “Mziki sio mgumu kama watu wanavyofikiria ila ugumu unatokana na wasanii kutokuwa wabunifu na kutunga mistari ambayo inakubalika “Alisema D.Doctor ambaye pia ni mwana familia wa kundi la Akili Music Group lenye maskani yake jijini Tanga.

Hata hivyo hakusita kuuzungumzia chanzo cha mziki huo kutokufika mbali ambapo alisema hali hiyo inachangiwa na wasanii kubweteka na kunakili nyimbo kutoka kwa wasanii wengine hali ambayo inadumaza mziki huo.

Msanii huyo hivi sasa anatamba na nyimbo mbalimbali ikiwemo “Salima” aliyoimba mahadhi ya Zuku,Mwache Alie na Ulivyo ambazo zote amezirekedia kwenye studi za Ganstar Record chini ya Mtayarishaji Danny.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »