D.DOCTOR :AWASAA WASANII KUWA WABUNIFU.
Na Oscar Assenga,Tanga.
WASANII wa mziki wa BongoFleva nchini wametakiwa kuwa wabunifu na kubadilika kutokana na mazingira ili kuendana na kasi ya maendeleo na kuutangaza mziki huo kitaifa na kimataifa kama ilivyokuwa kwa nchini nyengine duniani.
WASANII wa mziki wa BongoFleva nchini wametakiwa kuwa wabunifu na kubadilika kutokana na mazingira ili kuendana na kasi ya maendeleo na kuutangaza mziki huo kitaifa na kimataifa kama ilivyokuwa kwa nchini nyengine duniani.
Wito huo ulitolewa na Msanii wa mziki huo mkoani Tanga,Dominick
Mndeme “D.Doctor wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi ambapo alisema
kutokuwa na umakini kwa wasanii wengi
kumewafanya kutoka na kuonekana kuwika kwa muda fulani na baadae kupotea
kwenye tasnia hiyo kitendo ambacho kinachangia pia kushusha mziki huo.
Alisema licha ya kuwa mziki huo kupiga hatua kubwa sana hapa
nchini zipo changamoto mbalimbali ambazo zinawakabili ikiwemo kubaguliwa na
baadhi ya vyombo vya habari kuchezwa nyimbo zao kutokana na uchanga walionao
kwenye tansia hiyo.
“Mziki sio mgumu
kama watu wanavyofikiria ila ugumu unatokana na wasanii kutokuwa wabunifu na
kutunga mistari ambayo inakubalika “Alisema D.Doctor ambaye pia ni mwana
familia wa kundi la Akili Music Group lenye maskani yake jijini Tanga.
Hata hivyo hakusita kuuzungumzia chanzo cha mziki huo
kutokufika mbali ambapo alisema hali hiyo inachangiwa na wasanii kubweteka na
kunakili nyimbo kutoka kwa wasanii wengine hali ambayo inadumaza mziki huo.
Msanii huyo hivi sasa anatamba na nyimbo mbalimbali ikiwemo “Salima”
aliyoimba mahadhi ya Zuku,Mwache Alie na Ulivyo ambazo zote amezirekedia kwenye
studi za Ganstar Record chini ya Mtayarishaji Danny.