UVUNAJI WA MAZAO YA BAHARI UMEPUNGUA KUTOKA TANI 481 HADI TANI 316 MKOANI TANGA

January 10, 2014


 Tanga.
HALI ya uvunaji wa  mazao ya baharini katika mkoa wa Tanga imepungua kutoka tani 481 zilizopatikana mwaka 2011/2012 zenye thamani ya fedha za kitanzania 4,821,440,915.15 zilizosafirishwa nje ya nchini hadi kufikia tani 316 kwa mwaka 2012/2013 ambapo upungufu huo wa tani 165.

Hayo yalisemwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Luteni Mstaafu,Chiku Gallawa wakati akizungumza na TANGA RAHA BLOG ambapo alisema upungufu huo umesababishwa na hali ya soko la mazao kama Pweza kwa nchi Ulaya kupungua.


Gallawa alisema sekta ya uvuvi mkoani Tanga imeendelea kutunza mazingira ya uzalishaji wa mazao ya majini kwa kudhiti uvuvi haramu  ambapo mwaka 2011-2012 jumla ya doria 120 zilifanyika na  kufanikiwa kuwakamata wahalifu 20 na kuwafikisha mahakamani.

Licha ya kuwakamata watuhumiwa hao pia walikamata vyombo vya baruti 6  na baruti 10 na bunduki 5 za kuvulia zilikamatwa,Samaki wa baruti kilo 240 walikamatwa na kutekelezwa na makokoro  ikiwemo juya 60 ambavyo vilikuwa vikitumika kwenye uvuvi haramu.

Aidha alisema jumla ya kesi 22 zilifuatiliwa mahakamani ambapo kesi CC 06/2009 inayohusu mtu mmoja kwa kosa la kupatikana na samaki wa baruti ilitolewa hukumu ya kifungo cha miezi mitatu jela na kesi CC 363/09 inayohusu mtu mmoja kupatikana na samaki w baruti iliyotolewa hukumu ya kumuachia huru mshtakiwa  wakati kesi nyengine zilikuwa zikiendelea.


Mkuu huyo wa mkoa alisema katika kipindi cha mwaka 2012-2013 Jumla ya doria 44 zilifanyika na kesi 10 zilifuatiliwa mahakamani ambapo jumla ya vyombo vya baruti 20 vilikamatwa pamoja na sanmaki wa baruti 160 walikamatwa.

Aliongeza kuwa pia magari 20 yanayosafirisha mazao ya samaki kwenda mikoa mbalimbali yalikaguliwa ambapo kwenye mwaka huu mikuki,mishale ya kuchomea samaki 20 ilikamatwa ikiwemo makokoro na juya 5 zilikamatwa.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »