Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na watafiti kutoka
taasisi ya Utafiti wa Kilimo Uyole iliyopo Mkoani Mbeya walipomtembelea
ofisini kwake leo kutambulisha mpango wa SARD (Strategic Agriculture
Reseach Development) unaodhaminiwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika ADB
(Africa Development Bank). Mpango huo una lengo la kupunguza utegemezi
wa chakula nchini kwa kuongeza uzalishaji wa vyakula mbalimbali ikiwemo
zao la ngano ambalo ni sehemu ya mradi huo Mkoani Rukwa.
Katika
kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Rukwa alisisitiza juu upatikanaji wa masoko
ya kudumu kwa mazao yatakayozalishwa katika mpango huo badala ya
kuwekeza nguvu katika uzalishaji pekee.
Ndugu
Anthony Elanga mtafiti kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Uyole Jijini
Mbeya ambae pia ni Mratibu wa Utafiti wa Zao la Ngano Tanzania
akizungumza katika kikao hicho. Amesema mpango huo utahusisha wakulima
na vikundi vya wakulima ambao watapatiwa elimu na kuwezeshwa mikopo
mbalimbali ya kuendeleza kilimo cha ngano Mkoani Rukwa.
Mkutano ukiwa unaendelea.
(Na Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @rukwareview.blogspot.com)