Na Magreth Kinabo – Maelezo
Rais Jakaya
Kikwete amewataka Wakuu wa mikoa na wilaya kuhakikisha
kuwa wanasimamia Mpango Mkakati ulioboreshwa wa Kuongeza Kasi ya
Kupunguza vifo vya Uzazi vya wakinamama na watoto hususan wachanga ili
kutimiza malengo ya millennia namba nne na tano ifikapo mwaka 2015.
Aidha Rais Kikwete aliagiza viongozi wa mapango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) kuliingiza suala la afya katika mpango huo.
Changamoto hiyo imetolewa leo na
Rais Kikwete kabla ya kuzindua mpango huo, ulioenda sambamba na
uzinduzi wa kadi ya ufuatiliaji(scorecard) ambayo itakuwa inaonesha
tathimini na ya maendeleo na mkakati huo kwa kila mkoa na wilaya.
Rais Kikwete aliwataka wakuu hao
na watendaji wao kutoa ripoti ya kadi ya ufuatiliaji kila baada ya
miezi minne. Kadi hiyo, ambayo itakuwa na taarifa ya maendeleao ya
kupunguza vifo vya watoto wachanga, chini ya miaka mitano na
wakinawajawazito.
Uzinduzi huo, uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Mwalimu J.K. Nyerere jijini Dares Salaam.
Alisema vifo vya uzazi vya
wakina mama vimepungua kutoka 578 kwa vizazi hai 100,000 mwaka 2005 na
kufikia vifo 454 kwa vizazi hai 100,000 kwa sasa, wakati lengo la
milenia ni vifo 193 kwa vizazi hai 100,000.
“ Bado tuna safari ndefu
ninawataka wakuu wa mikoa na wilaya kuchulikia jambo hili kwa umakini na
kulipa kipaumbele kwani jukumu hili si la waganga wakuu wa mikoa au
wilaya na mimi nitakuwa ninafuatilia kwa kuwa jambo hili, lipo mikononi
mwangu. Ninataka kulifuatialia kabla sijamaliza kipindi cha uongozi
wangu,” alisema Rais Kikwete.
Aliongeza kuwa vifo hivyo vya
wakina mama na watoto hutokea lakini havifatiliwi ndio maana inakuwa
vigumu kubaini njia za kuvipunguza.
“ Baya zaidi wanakufa kwa sababu
zinazoweza kuzuilika, kadi ya ufuatiliaji ikifuatiliwa na wakuu wa
mikoa itasaidia kupunguza vifo,” alisisitiza.
Alisema ikiwa watoto waliochini
ya miaka mitano na wakinamama wajawazito watazingatia masuala ya lishe
bora kwa kipindi cha siku 1000 pia itasaidia kupunguza vifo hivyo.Huku
akisema vyakula hivyo vipo majumbani kinachohitajika ni elimu.
Aliwataka wakimama kuzingatia
uzazi wa mpango(nyota ya kijani ) ili kusaidia kupunguza tatizo hilo,
pia kushirikisha wanaume juu ya jambo hilo.
Rais Kikwete pia alisema
asilimia 51 ya wakina wanaojifungua huhudumiwa na watalaamu wenye ujuzi,
wakati malengo ya milinea ni asilimia 80, hivyo bado kuna
changamoto ya asilimia 29.
Kwa Upande wake Naibu Waziri
wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe, alisema
kwa kipindi cha mwaka huu wanampango wa kuajiri watalaamu hao 11,021.
Alisema Tanzania imefanikiwa
kutimiza lengo la milinea namba nne kabla ya wakati kwa kupunguza vifo
vya watoto chini ya miaka mitano kwa kiwango cha 54 kwa watoto
wanaozaliwa 1000, kutoka 165 kwa wataoto wanaozaliwa 1000 mwaka 1990.
Alizitaja nchi nyingine zilizofanikiwa ni Rwanda, Malawi,Ethiopia
Rwanda na Malawi.
Naye mwakilishi wa wakuu hao,
Dk. Christine Ishengoma alisema uwajibikaji wa viongozi na
watendaji ni jambo la muhimu katika kutekeleza mpango huo, hivyo suala
hilo linawezekana.
Kaimu Katibu Mkuu wa Ofisi ya
Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Dk. Deo
Mutasiwa alisema sheria ndogondogo zinatengenezwa ili kuwezesha mpango
huo kufikia lengo.
Dk. Mutasiwa alizitaka
halimashauri kutumia vyanzo vyake vya mapato ya ndani kwa asilimia 60
kuwekeza katika masuala ya afya, elimu maji na barabara za vijijini.
Alisema hivi sasa wako katika
mchakato wa kupata kibali cha kuwaezesha watoa huduma wa afya wanaomba
nafasi za kazi kufanyia kazi maeneo wanayotoka.
EmoticonEmoticon