KIUNGO
Samir Nasri ameendeleza wiki nzuri za mafanikio katika soka, baada ya
jioni ya leo kufanya kazi nzuri Manchester City ikicheza mchezo wa
kirafiki na Al Ain katika ziara yake ya Falme za Kiarabu.
Mfaransa
huyo atakwenda na kulala na tabasamu zuri baada ya kutengeneza mabao
mawili katika ushindi wa 3-0 wa mabingwa hao wa Ligi Kuu ya England
kwenye Uwanja wa Hazza bin Zayed.
Anakwenda na mpira: Nyota wa Manchester City, Samir Nasri akimtoka beki wa Al Ain katika mchezo wa kirafiki leo
Akiwa
na machungu ya kutemwa na kocha Didier Deschamps katika kikosi cha
Ufaransa cha Kombe la Dunia, Nasri alipambana kuhakikisha anawaziba
midomo wanaomkandia baada ya demu wake, kutweet matusi dhidi ya timu ya
taifa.
Ameacha
miguu yake izungumze, akiwapasia mipira ya kufunga Marco Lopes dakika
ya 63 na Stevan Jovetic dakika ya 78 katika me chi ambayo wenyeji
walibadilisha wachezaji 25.
Bao
lingine la City lilifungwa na Hiwula kwa penalti dakika ya 89 katika
mechi iliyohudhuriwa na watu 21,437. Al Ain ndiyo klabu yenye mafanikio
zaidi kihistoria UAE na Jumapili itacheza Fainali ya Kombe la Rais. 
Marcos Lopes akishangilia bao lake dhidi ya Al Ain
Mwenye timu: Mmiliki wa Manchester City, Sheikh Mansour bin Zayed Al Nahyan akipiga makofi Uwanja wa Hazza bin Zayed leo

EmoticonEmoticon