*VITA KALI YA MASAA MATANO CHATU NA MAMBA, MAMBA HOI ATOLEWA MAJINI NA KUMEZWA
Nyoka aina ya Chatu akipambana na Mamba ndani ya maji.
Nyoka huyo baadaye alifanikiwa kumzidi nguvu Mamba na kumuua na kisha kumtoa ndani ya maji hadi nchi kavu na kuanza kummeza.
******************************************
Katika
hali isiyokuwa ya kawaida na isiyotarajiwa na wengi, Nyoka mkubwa aina
ya Chatu ameibuka na ushindi kwa kumsinda nguvu Mamba akiwa ndani ya
maji na kisha kumtoa nchi kavu na kummeza, huko Kaskazini mwa mji wa
Queens Land.
Tukio
hilo lililotokea juzi lilivuta hisia za watu wengi walioshuhudia vita
hiyo, katika ziwa Moondarra lililopo karibu na mlima Isa, ambapo baadhi
ya walioshuhudia tukio hilo walivutiwa na vita hiyo na kuanza kunasa
tukio hilo katika kamera zao.
Imeelezwa
kuwa nyoka huyo aliyekuwa na urefu wa Futi 10, alijipinda na
kujiviliga kwenye mwili wa Mamba na kupambana naye na kisha kumtoa
majini na kuanza kummeza, ambapo Chatu huyo alitumia dakika 15 kumla
Mamba huyo hadi kummeza baada ya mpambano wao uliochukua kiasi cha masaa
matano, huku wote wakionekana kuchoka.