Matukio Bunge la Katiba Leo
Wajumbe
wa Bunge Maalum la Katiba Jenista Mhagama (Kushoto) ambaye pia ni Naibu
Waziri Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Bi. Christowaja Mtinda
wakiwasili katika ukumbi wa bunge kwa ajili ya Semina ya uundwaji wa
kanuni za kuongoza Bunge Maalum la Katiba leo Mjini Dodoma.
Wajumbe
wa bunge maalum la Katiba Jumanne Maghembe ambaye pia ni Waziri wa Maji
akiwa na Vita Kawawa, Mbunge wa Namtumbo wakiwasili katika ukumbi wa
Bunge kwa ajili ya Semina ya uundwaji wa kanuni za kuongoza Bunge Maalum
la Katiba leo Mjini Dodoma.
Mjumbe
wa Bunge Maalum la Katiba ambaye pia ni Waziri Waziri wa Ushirikiano wa
Afrika Mashariki Samweli Sitta akimweleza jambo Mjumbe wa Bunge hilo
ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu Steven
Wassira( Kulia). Leo Mjini Dodoma. Chini yao ni wajumbe wa Bunge Hilo
Seif Khatibu( Kushoto) na Anna Makinda ambaye pia ni Spika wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mjumbe
wa Bunge Maalum la Katiba ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais
Mahusiano na Uratibu Steven Wassira akiwaeleza jambo Wajumbe wa Bunge
hilo leo Mjini Dodoma
Mjumbe
wa Bunge Maalum la Katiba ambaye pia ni Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akimwelekeza jambo
Mtangazaji wa TBC ONE Bw. Shaaban Kissu wakati akiwasili katika katika
ukumbi wa Bunge leo Mjini Dodoma.