MAN UNITED WAKALISHWA 3-0 NA LIVERPOOL OLT TRAFFORD, GERRARD ALMANUSRA APIGE HAT-TRICK!!

March 16, 2014
LIVERPOOL kwa mara ya kwanza ndani ya miaka mitano iliyopita wamepata ushindi katika dimba la  Old Trafford baada ya kuwafumua wenyeji Manchester United mabao 3-0.
Nahodha mashuhuri wa Liverpool na timu ya Taifa ya Uingereza, `Mr. Liverpool`,  Steven Gerrard alifunga mabao mawaili, huku bao la tatu likitiwa kambani na Luis Saurez.
Gerrard alifunga kwa penati dakika ya 34 baada ya Rafael kuushika mpira kwa mkono, na alifunga penati nyinginie dakika ya 46 kufuatia Phil Jones kumfanyia madhambi Joe Allen eneo la hatari.
Nyota huyo wa England angefunga mabao matatu `Hat-Trick` katika dimba la Old Trafford tangu mwaka 1936 endapo angefanikiwa kutia kambani penati ya tatu waliyopewa dakika ya 79 baada ya Nemanja Vidic kumfanyia madhambi Daniel Sturridge, lakini alikosa penati hiyo.
Vidic alitolewa nje kwa kadi nyekundu, lakini  penati ya tatu inaonekana haikuwa halali kwani Sturridge alionekana katika video akimdanganya mwamuzi na kushinda janja yake.
Kikosi cha Man Utd leo: De Gea 6, Rafael 5,Jones 5, Vidic 5, Evra 5.5, Fellaini  5 (Cleverley 76, 6), Carrick 5, Mata 4.5 (Ferdinand 87), Rooney 4.5, Januzaj 5 (Welbeck 76, 6), Van Persie 4.5.
Kikosi cha Liverpool: Mignolet 7, Johnson 7, Skrtel 8, Agger 7.5, Flanagan 7.5, Henderson 7.5, Gerrard 8.5 (Lucas 87), Allen 8, Sterling 6 (Coutinho 72, 6), Sturridge 8, (Aspas 90+1), Suarez 8.
Unbelievable: Luis Suarez celebrates after scoring the third in the 3-0 win at Old Trafford
 Hawaamini: Luis Suarez akishangilia bao la tatu alilofunga katika ushindi wa  3-0 uwanjani  Old Trafford
Mind the gap: Liverpool are now 14 points clear of United and just four points off leaders ChelseaPengo kubwa: Liverpool sasa wapo mbele kwa pointi 14 dhidi ya Man United na pointi 4 nyuma ya vinara Chelsea.
Slotted home: Suarez scores to round off the 3-0 victory and put Liverpool to within four points of ChelseaAmewazamisha kwao: Suarez akifunga bao lake katika mchezo wa leo
Contrast: Suarez gives his side the thumbs up as Wayne Rooney complains to his team-matesTofauti:  Suarez  akiwapa dole wenzake kwa kazi nzuri, wakati huo huo Wayne Rooney anawalaumu wenzake
Togetherness: Liverpool were outstanding at Old Trafford, despite United's indisciplineKwa pamoja: Wachezaji wa Liverpool wakishangilia ushindi wao
Up and down: United are now 14 points behind Liverpool, who are now major contenders for the titleAibu kubwa: United wapo nyuma kwa pointi  14  dhidi ya Liverpool, ambao sasa wanaonekana washindani wa ubingwa msimu huu

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »