Na Oscar Assenga,Tanga.
RAIS wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania,Jakaya Mrisho anatarajiwa kuwasili mkoani Tanga kesho kwa lengo la kuzindua mradi wa kanda maalumu ya uwekezaji katika eneo la viwanda Pongwe wenye ukubwa wa eneo la mradi ni hekta 67.7 kwa viwanda na hekta 4.3 kwa eneo la makazi.Akizungumza na waandishi wa habari jana,Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Luteni Mstaafu,Chiku Gallawa alisema mradi huo wa kanda maalumu ya uwekezaji ni mradi ulioanzishwa na Tanga Economic Corridor Limited(Industrial Park Developer)ambayo ni kampuni inayoundwa kwa ubia kati ya halmashauri ya jiji la Tanga yenye hisa 48 asilimia na (Good PM group LTD through Africa Future)yenye hisa 51 asilimia) ambayo ni taasisi isiyo ya kiserikali inayowezesha uendelezaji wa miundo mbinu africa.
Alisema makubaliano yaliyopo ni halmashauri ya Jiji la Tanga kuchangia eneo na Good PM Group Limited kuwekeza katika miundo mbinu ambapo mradi mzima unatarajiwa kugharimu kiasi cha shilingi za kimarekeni milioni 277 kati ya hizo shilingi za kimarekani milioni 40 zitatumika kwa kuendeleza miundo mbinu na shilingi za kimarekani milioni 237 zitatumika kwa uwekezaji wa moja kwa moja kutoka kwa viwanda vyote.
Mkuu huyo wa Mkoa alisema baada ya mradi huo kukamilika unatarajiwa kutoa fuksa za ajira kwa vijana zaidi ya 2,000 katika viwanda 17 vinavyotarajiwa kujengwa mkoani hapa ili kuweza kuleta maendeleo kwa wakazi wa mkoa na wilaya zake.
Aidha mkuu wa mkoa wa Tanga aliwataka wananchi wote kujitokeza kwa wingi kumlaki mheshimiwa Rais katika uwanja wa ndege tanga kuanzia saa 4.00 asubuhi na kushiriki katika uzinduzi wa mradi huo utakaofanyika kata Pongwe katika halmashauri ya Jiji la Tanga.
Mwisho.
EmoticonEmoticon