UHURU seleman arudi Nyumbani”

June 20, 2013

Na Oscar Assenga, Tanga.

UONGOZI wa Klabu ya Coastal Union ya Tanga “Wagosi wa Kaya” umeingia mkataba wa mwaka mmoja na kiungo mshambuliaji Azam Fc  ,Uhuru Selemani kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo msimu ujao.

Athibitisha habari hizi,Mwenyekiti wa Klabu ya Coastal Union ya Tanga, Hemed Aurora “Mpiganaji”ni kweli wamefanya hivyo na kueleza ujio wa mchezaji huyo utaleta chachu na ushindani katika kikosi hicho ambacho kinatarajiwa kuwa tishio katika medani ya soka hapa nchini.

Aurora alisema makubaliano ya mkataba huo yaliafikiwa jana na kukubaliana na mchezaji huyo ili aweze kuitumikia timu hiyo katika msimu ujao wa ligi kuu Tanzania bara ambapo alieleza wao kama uongozi wa klabu hiyo wamefarijika sana na ujio wake.

Alisema Uhuru ni miongoni mwa wachezaji wapya waliosajiliwa na klabu hiyo msimu huu wengine ambayo tayari wameshasaini kuichezea klabu hiyo ni Haruna Moshi “Boban” na Juma Nyoso ambayo ni wachezaji wenye uzoefu mkubwa ambao wataweza kuwa kuleta upinzani mkubwa.

Aidha Aurora alisema klabu hiyo itaendelea kuwa na msimamo wake wa kuwasajili wachezaji ambao hawana majina ili waweze kushirikiana na wachezaji wachache ambao wamewasajili wenye majina makubwa na uzoefu wa kisoka hapa nchini.

Aliongeza kuwa hivi sasa nguvu zao wanazielekeza kwa wachezaji wachanga ambao hawana majina makubwa kwenye medani ya soka kwani wanaamini wachezaji wachanga wanauwezo mkubwa wa kuifanya timu hiyo ipate mafanikio.

Akizungumzia tetesi zilizozagaa kuwa wana mpango wa kumchukua mlinda mlango Juma Kaseja ,Aurora alisema mpango huo kwa sasa hawana kutokana na kuwa na makipa wazuri watatu ambao wataitumia klabu hiyo msimu ujao.

Aliwataja makipa hao kuwa ni Mlinda mlango nambari moja Shabani Kado, Said Rubawa ambaye alikuwa mlinda mlango wa JKT Oljoro ya Arusha na Ally Mansour ambaye aliidakia timu hiyo katika mechi za uhai Cup akiwa na kikosi cha pili cha timu hiyo chini ya umri wa miaka 20.

Mwisho

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »