Na Oscar Assenga,Tanga.
Baraza la Wakulima Tanzania limeeleza kusikitishwa kwake nas namna ambavyo Bajetion ya serikali iliyosomwa hivi karibuni ilivyoendnelea kuwapuuza wakulima pamoja na Baraza hilo kupeleka mapendnekezo yao kwa serikali.
Mwenyekiti wa Baraza hilo, Salum Shamte akitoa maoni ya
Baraza katika mahojiano na vyombo vya
Habari alisema kuwa Bajeti ya mwaka huu, pamoja kutangaza neema kwa kuanza kwa
Benki ya Wakulima ambayo ilikuwa kilio kikubwa cha wakulima, bado haijagusa
masuala nyeti kwa wakulima kama vile suala la muda mrefu la kupunguza mzigo wa
kodi kwa nia ya kuwawezesha wakulima kuongeza tija, uwekezaji, mapato na
hatimaye kuondo umaskini.
“Kodi hizo maranykingine zinaongezwa kineyemela na kimya
kimya bila serikali kufanya majadiliano na wadau,” alilalamika Mwenyekiti huyo.
Alisema kuwa kama Tanzania inataka kuleta mapinduzi ya
kijani katika kilimo lazima iwe makini katika suala la kuondoa kero ya kodi
nyingi kwa wakulima na wazalishaji wengine.
Shamte alitoa mfano wa ushuru wa mazao unatozwa na
halamshauri za serikali za mitaa ambao alisema wakuilma wamalazimika kulipa
ushuru wa asilimia 5 ambao ni mara 17 zaidi ya wenye viwanda ambao hulipa ushuru
wa huduma wa aslimia 0.3. “Hii haieleweki, haielezeki na haikubaliki,” alisema
Mwenyekiti huyo.
Alibainisha kuwa Baraza limefanya utafiti kuta kujua kama
mapato hayo yanayopkusanya na Halmshauri yanafika katika hazina za halmashauri
hizo. “NI asilimia 67 tu ya makusanyo hayo ya ushuru ambayo yanafika
halmashauri na fedha nyingine zinayeyuka kastika mifuk ya wajanja,’ alieleza.
Alisema serikali lazima isikie kilio cha wakulima na kuchukua
hatua kuhus kodi hiyo kwa mujibui w a maepndekezo ili kuleta tija wa wakulima.
Shamte pia alieleza kuhusu kupanda kwa kiasi kikubwa kwa
kodi ya aardhi mwaka jana mwezi Agosti ambapo kodi hiyo imepnda kwa asilimia
500 kutoka Sh. 200 kwa hekta hadi Sh. 1,000 ka hekta kwa walioko maeneo ya
vijijini na Sh. 10,000 kwa hekta kwa mashamba ambayo yako maeneo yaliyoko chini
ya mamlaka za miji kwa wale ambao wana hati.
Alisema kuwa kodi hiyo hailipiki kwa sababu kama wakulima
watalipa kodi hiyo na nyingine zinazowakabili basi watafunga shughuli zao. Alitoa
mfano wa Ranchi ya Ruvu ambayo alisema hivi sasa inatakiwa kulipa Sh. milioni 107
kwa mwaka hata kabla hawajaanza kuuza
ndama.
Akizungumzia mkonge, Shamte ambaye pia ni Mkrugenzai
Mtendaji wa Kampuni ya Mkonge wa Katani Limited ya Tanga, alisema kuwa sekta ya
mkonge italazimika kulipa jumla ya Sh.Bilioni 1.18 kwa mwaka kama kodi ya ardhi
kutoka Sh. Milioni 87 iliyokuwa ikilipa awali.
Pia alizungumzia ongezeko la kutisha la kodi ya OSHA ambayo
imepandishwa kutoka Sh. 5,000 kwa mfanyakaazi hadi Sh. 40,000 kwa mfanyakazi
kwa mwaka jambo ambalo kwa mfano katika sekta ya mkonge itaifanya ilazimike
kulipa jumla ya Sh. Bilioni 14 kwa mwaka kwa ajili ya kodi hiyo tu.
Alitaja pia kodi ya huduma za zimamoto ambayo imepanda
kutoka Sh. 200,000 kwa mwaka hadi kufikia Sh. milioni 2 kwa mwaka . alisema
kuwa kdo hiyo kwa mashamba mengi haina maana sana kwa sababu yako mabli sana na
huduma hiyo.
Shamte pia alilalamikia ongezeko la mamfuta ya diseli ambayo
amesema kuwa ndio roho kwa kwa sababu hahwatumii mafuta hayo kwa usairishaji tu
bali katika utayaruishaji wa mashamba, jambao ambalo litaongeza gharama za
uendeshaji wa mazao na kuua faida kwa wakulima pamoja na kushindwa katika ushindani na bidhaa kama hizo katika soko la
kimataifa.
Alisema kuwa katika nchi nyingine kilimo kinapewa upendeleo fulani
kwa kuondoa kodi kanma hizo ili kuongoeza tija.
Mwenyekiti huyo, wakati huo aliitaka serikali kuhakikisha
kuwa inapopunguza kodi jambo hilo linatekelzw ipasavyo. Alitoa mfano kuwa nmawka
jana serikali ilipunguza kodi kwa vipuri lakini hadi hivi kodi hiyo inaendele kutozwa.
MWISHO
EmoticonEmoticon