Na Mwandishi Wetu
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira ikiongozwa na Mwenyekiti wake Jackson Kiswaga imetoa pongezi kwa Mamlaka ya majisafi na Usafi wa Mazigira Tanga ,wakati wa kazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maji mkoani hapo .
Kamati hiyo imekagua chanzo cha maji cha Mabayani ambacho ni chanzo kikubwa kunacho hudumia jiji la Tanga na mtambo wa kutibu na kuzalisha maji wa Mowe
Mwenyekiti wa Kamati Kiswaga amesema lengo la ukaguzi huo ni kuona namna fedha zilizotolewa na serikali zinavyotumika katika kutekeleza miradi ya maji
“Wananchi tuwape maji na utekelezaji wa mradi wa hatifungani uanze haraka ili kutimiza azma ya Rais ya Kumtua mama ndoo ya maji kichwani," Kiswaga amesema.
Ameipongeza Wizara ya Maji na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tanga .Tanga -UWASA kwa kazi wanayoifanya katika kuwapeleka huduma ya maji wananchi ili kuondosha tatizo la uhaba wa maji katika jiji la Tanga .
Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso (Mb) akiishukuru kamati amesema maji yatakayo zalishwa kupitia mradi wa hati fungani utaweza kuhudumia na maeneo ya jirani hivyo jukumu la Wizara ya Maji ni kusimamia kuanza kwa mradi huo ukamilike kwa wakati uliopangwa ili kuhakikisha azma ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa wananchi inatekelezeka.
EmoticonEmoticon