TIB BENKI YAPONGEZWA KWA KUTOA HUDUMA NZURI MAONESHO YA AFRIKA MASHARIKI

September 13, 2024

 Waziri wa Viwanda na Biashara, Mheshimiwa Dkt. Selemani Saidi Jafo, ameipongeza Benki ya maendeleo TIB kwa kuibuka mshindi wa pili katika kipengele cha Watoa Huduma za Kibiashara kwenye Maonesho ya 19 ya Biashara ya Afrika Mashariki yanayoendelea kwenye Viwanja vya Furahisha Jijini Mwanza.

Maonesho hayo yenye kauli mbiu "Uboreshaji wa mazingira ya uwekezaji na biashara ni kichocheo katika kukuza uchumi wa Nchi", yalianza rasmi tarehe 6 Septemba na yanatarajiwa kukamilika tarehe 15 Septemba 2024 na yametoa fursa kwa wafanyabiashara kutoka mataifa ya Afrika mashariki kunadi bidhaa mbalimbali zinazozalishwa kwenye ukanda huo.

Baada ya kukabidhiwa Cheti na Waziri Jaffo wakati wa uzinduzi wa Maonesho hayo Meneja wa Benki hiyo ya TIB Kanda ya Ziwa, Bw. Zacharia Kicharo, alipo fanya mazungumzo na mwandishi wetu, amesema benki yao imekuwa ikifanya kazi kwa kushirikiana na taasisi za umma na zile za binafsi pia inafanya kazi kwa kuwawezesha mikopo wakulima wadpgo, wa kati na wakubwa.

Akiwakaribisha wananchi kutembelea maonesho hayo ya biashara ya afrika mashariki Bwana Kicharo amesisitiza kuwa zipo fursa nyingi kwa wajasiriamali na wananchi kwa ujamla watakazo zipata pindi watakapo tembelea banda la TIB.

“kuna elimu ya masuala ya kiuchumi na biashara inayo tolewa hapahapa bandani kwetu na maafisa wetu hivyo ni muhimu kufika kwa na kujipatie elimu hii hususani kwa wakaazi wa Mwanza na kanda ya ziwa” alisema 

Kwa kuzingatia eneo la kimkakati la kanda ya ziwa hususani katika sekta ya uchimbaji madini na biashara ya madini ,Benki ya maendeleo ya TIB kupitia tawi lao la kanda ya ziwa inahudumia mikoa ya Kigoma, Tabora, Shinyanga, Geita, Kagera, Simiyu na Mwanza yenyewe lilipo tawi la benki hiyo kwa kanda ya ziwa, na kwenye maonesho ya biashara ya Afrika Mashariki wameweka banda linalotoa huduma za benki hiyo kwa wananchi na wajasiriamali wa kada zote wanao fika viwanja vya furahisha yanapo fanyika maonesho hayo.

Pichani ni Mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa Maonesho ya 19 ya Biashara ya Afrika Mashariki yanayoendelea Jijini Mwanza, Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Selemani Jaffo, akimkabidhi Meneja wa Benki ya Maendeleo TIB, Kanda ya Ziwa,  Zacharia Kicharo, cheti na zawadi ya mshindi wa pili katika kipengele cha Watoa Huduma za Kibiashara. Maonesho haya yenye kauli mbiu "Uboreshaji wa mazingira ya uwekezaji na biashara ni kichocheo katika kukuza uchumi wa Nchi", yalianza tarehe 6 Septemba na yanatarajiwa kukamilika tarehe 15 Septemba 2024.
Benki ya Maendeleo TIB inashiriki kwenye Maonesho hayo Kwa Kutoa Elimu ya Huduma mbalimbali inaayotolewa na Benki hiyo.


Share this

Related Posts

Previous
Next Post »