DC TANGA AIPONGEZA FIVE BROTHERS KWA KUANZISHA MASHINDANO YA REDE

February 28, 2018
MKUU wa wilaya ya Tanga ,Thobias Mwilapwa kulia akimkabidhi Kombe la Ubingwa wa Mashindano ya Rede Nahodha wa  timu ya Magomeni Sisters
Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa kulia akimkabidhi kombe  mshindi wa pili ambao ni Mkwakwani Baisket
  Mabingwa wa Mashindano ya Rede ambao ni timu ya Magomeni Sisters wakiwa na kombe lao mara baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa
 Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akizungumza wakati akifunga mashindano hayo yaliyofanyika kwenye viwanja vya CCM Mkwakwani mjini Tanga
 Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa kulia akimkabidhi Cheti cha kutambua mchango wake katika mashindano hayo Dj
 Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa kulia akimkabidhi Cheti cha kutambua mchango wake katika mashindano hayo Dj Bad Fuvu
 Sehemu ya Majaji wa Mashindano hayo wakiwa kazini
 Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa wa pili kutoka kulia akiwa na Muandaaji wa mashindano ya Rede Nassoro Makau kushoto kutoka ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Five kulia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga  Faidha Salim
 Timu ya Magomeni Sisters wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa na wageni wengine wakiwemo waaandaaji wa mashindano hayo
 Sehemu ya timu ambazo zilikuwa zikishiriki mashindano hayo wakiwa na mashabiki wakifuatilia mechi ya fainali
MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa ameipongeza Kampuni ya Five Brothers kwa kuonyesha ubinifu mkubwa kuanzisha mashindano ya mchezo wa rede ambayo imesaidia kurudisha michezo ya zamani iliyokuwa ikipendwa.
Pongezi hizo zilitolewa mwishoni mwa wiki wakati akifunga fainali za mashindano hayo ambapo mshindi wa kwanza alikuwa ni timu ya Magomeni Sisters ambao walizawadiwa fedha taslimu 120,000 kikombe cha mashindano hayo, medali, unga wa ngano kilo 25 na mafuta lita 10.
Huku mshindi wa pili ambao ni Mkwakwani Baisket iliweza kupata kitita cha sh.70,000,medali,ngano kg 5 na mafuta lita 5 ambazo zilitolewa na mgeni rasmi katika mashindano hayo.
Alisema kimsingi uanzishwaji wa mashindano hayo umekuwa ni chachu kubwa kuweza kujenga umoja na mshikamano kwa vijana kuweza kutumia michezo kama sehemu ya kuimarisha miili yao na kujiepusha na vitendo viovu kwenye jamii.
“Ubunifu huu ambao ulionyesha wakati wa michuano hii ya rede ni mzuri na unapaswa kuendelezwa kila mwaka na sisi tutaendelea kuwaunga mkono kwa kuhakikisha yanafanyika kwa waledi mkubwa “Alisema.
Awali akizungumza, Mratibu wa Mashindano hayo kutoka Kampuni ya Five Brothers,Nassoro Makau alisema mchezo wa rede ni miongoni mwa michezo ambayo ilikuwa imesahaulika kwa kipindi kirefu hivyo wakaona wairudishe ili kuweza kuinua vipaji vinavyopatikana kupitia mchezo huo.
“Kwa kweli sisi kama Kampuni ya Five Brothers tumeona na kudhamiria kwa dhati kuona namna ya kurudisha michezo ya asili ambayo  ni pendwa kwa mkoa wa Tanga kwa kuipa thamani kwani mchezo kama ukuti ukuti na rede ni michezo ya asili hivyo tunapoirudisha tunasaidia kurudisha enzi na kuwakumbusha watu mambo mengi “Alisema Makau.
Alisema msimu huu mashindano hayo yalianza February 8 mwaka huu kwa mtindo wa ligi kwa kushirikisha timu 11 za jiji la Tanga na yamesaidia vijana kushiriki kwa kuonyesha vipaji vyao.
Naye kwa upande wake,Mwenyekiti wa Kongamano la Vijana na Balozi wa Vijana Mkoa wa Tanga,Selemani Mssey alisema mchezo huo utasaidia kuondoa vitendo vya umbea na kusutana kwa wasichana.
“Tanga wasichana walikuwa wakiongoza kusuta lakini uanzishwaji wa mashindano hayo utasaidia kuondoa hali hiyo pia kutoa fursa kwao kutumia michezo kama sehemu ya kuimarisha miili yao lakini kupata kipato “Alisema.
Prof. Elisante Ahudhuria Mkutano wa kuboresha Mazingira Ya Biashara EAC

Prof. Elisante Ahudhuria Mkutano wa kuboresha Mazingira Ya Biashara EAC

February 28, 2018

EL1
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwezeshaji, Prof. Elisante Ole Gabriel, (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe waliohudhuria kwenye Mkutano wa kuboresha mazingira ya Biashara kwenye Jumuiya ya Afrika ya Mashariki. 
EL2
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwezeshaji, Prof. Elisante Ole Gabriel, (kulia) akiagana na Makamu wa Rais wa Uganda, Mhe. Edward Sekandi (kushoto) kwenye Mkutano wa kuboresha mazingira ya Biashara kwenye Jumuiya ya Afrika ya Mashariki. Mhe. Sekandi ndiye alikuwa Mgeni Rasmi na ndiye aliyefungua Mkutano huo unaofanyika kwenye Hoteli ya Munyonyo, Nchini Uganda kuanzia tarehe 28 Februari hadi 01 Machi, 2018.
MCHUNGAJI SIMALENGA AWATAKA WANADAMU KUJIANDAA KABLA YA KIFO

MCHUNGAJI SIMALENGA AWATAKA WANADAMU KUJIANDAA KABLA YA KIFO

February 28, 2018

????????????????????????????????????
Mchungaji Augustino Simalenga wa Kanisa la TAG Kivule leo maeneo ya Kitunda akiombea mwili wa marehemu Jerome Swai aliyekuwa Fundi Sanifu Mkuu wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), kabla ya kusafirishwa kwa mazishi yatakayofanyika kesho wilayani  ya Rombo.
????????????????????????????????????
Msemaji wa familia ya marehemu Jerome Swai aliyekuwa Fundi Sanifu Mkuu wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Silvester Shayo (kulia) akitoa shukrani  kwa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Wafanyakazi wa TAA na watu wote walioshiriki kwenye msiba huo. Marehemu Swai atazikwa kesho wilaya ya Rombo.
????????????????????????????????????
Afisa Utumishi Mkuu wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Priscus Mkawe akisoma wasifu wa marehemu Jerome Swai aliyekuwa Fundi Sanifu Mkuu wa JNIA, kabla ya kuagwa nyumbani kwake Kitunda na kusafirishwa kwenda Rombo kwa mazishi yatakayofanyika kesho.
????????????????????????????????????
Kaimu Mkurugenzi wa  Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Johannes Munanka akiaga mwili wa aliyekuwa Fundi Sanifu Mkuu wa JNIA, Bw. Jerome Swai, ambaye atazikwa kesho wilayani Rombo.
????????????????????????????????????
Bi. Honoratha Emmilian ambaye ni mke wa marehemu Jerome Swai aliyekuwa Fundi Sanifu Mkuu wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), akilia kwa uchungu wakati wa kuuaga mwili wa mumewe nyumbani kwake Kitunda. Marehemu atazikwa kesho wilayani Rombo.
????????????????????????????????????
Ndugu wa marehemu Jerome Swai wakiuaga mwili wa mpendwa wao leo nyumbani kwake Kitunda, ambapo anatarajiwa kuzikwa kesho wilayani Rombo. Swai alikuwa Fundi Sanifu Mkuu wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).
????????????????????????????????????
Mkurugenzi wa zamani wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Prosper Tesha (mwenye miwani mbele) akijumuika na waombolezaji kwenye msiba wa aliyekuwa Fundi Sanifu Mkuu wa Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Jerome Swai aliyefariki Jumatatu ya wiki hii na atazikwa kesho wilayani Rombo.
swai-8
Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Fundi Sanifu Mkuu wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Jerome Swai likipandishwa ndani ya basi tayari kwa safari ya kwenda Rombo kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika kesho. Marehemu aliajiriwa mwaka 1984.
……………..
Na Mwandishi Wetu
MCHUNGAJI wa Kanisa la TAG Kivule, Augustino Simalenga amewataka wanadamu kujiandaa na kumrudia muumba wao kwani hawajui siku wala saa watakapokufa.
Alitoa kauli hiyo leo kwenye misa ya kumuaga marehemu Jerome Swai aliyekuwa Fundi Sanifu Mkuu wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), iliyofanyika nyumbani kwake maeneo ya Kitunda, ambapo amewataka watu kujiandaa mapema kwa kuwa hawajui watakapokwenda baada ya kifo.
“Neno la Mungu linatukumbusha kuwa tujiandae mapema, ndugu yetu Jerome ameshamaliza kazi, tunatakiwa kujitafakari sisi hatima yetu itakuwaje, kwani wapo waliolala mauti Biblia inasema hao wanapumzika wakisubiri siku atakaporudi Mwana wa Adam atakuja kuwachukua wote waliohai na wale waliokufa wakimuamini Kristu watafufuliwa kwanza ili kwa pamoja wamlaki Bwana wao mawinguni,” alisema Mchungaji Semalenga.
Alisema kila mtu atafakari maisha ya hapa duniani kwani mlango wa kutokea hapa duniani aidha ni kifo au siku Bwana atakapokuja kuchukua watu wake, hivyo ni vyema kujiandaa kwa kutafakari maisha baada ya hapa kwa sasa kuanza kujitengenezea hazina mbinguni.
“Ukisoma kitabu cha Mhubiri sura ya 3 utaona Mungu ameweka kila kitu na wakati wake, upo wakati wa kula na wakati wa kusema, wakati wa kunyamaza, wakati wa kuzaliwa na wakati wa kufa kila kitu kinawakati hata sisi tuliohai ni wakati wetu kuwa hai bali utafika wakati hatutaweza kuwa hai siku zote, na kila jambo lina mwanzo na mwisho, lakini mwisho wa jambo unatengenezwa wakati wa sasa kama maisha yetu ya sasa hatufikiri mwisho basi tukifika mwisho tutakuwa watu wa kujuta, watu wa kuomboleza na lakini sasa Mungu anatupa nafasi ya kuyakabili mambo yanayokuja na hatima ya maisha yetu,” alisisitiza.
Alisema katika kitabu cha Zabuni, kinasema binadamu amepewa maisha mafupi na machache, na kuishi ni miaka 70 na wachache wanaweza kuishi zaidi ya hiyo, ambapo ni tofauti na wanadamu wa kwanza waliishi miaka 100 ambayo nayo yalikuwa mafupi. Hata hivyo alisema baada ya kifo yapo maisha ya milele, ambayo mwanadamu anatakiwa kuyatafakari sasa kwa kujiwekea hazina itakayomwezesha kuishi vyema mbinguni.
Mchungaji Simalenga alisema amefanya utafiti katika huduma anazotoa lakini amegundua hakuna mwanadamu anayetaka kwenda jehanamu, hata asiyefanya ibada kwa Mungu anamatumaini ya kwenda mahala pema peponi.
“Mungu ameweka utaratibu na Mwanadamu akiuufuata ndio atafikia kwenye ule mpango ambao Mungu ameuweka, sasa kama hataki kuufuata anajikuta siku za maisha yake atajikuta mahala asipotaka kwa kilio, kujuta na kuomboleza, kwani alikuwa akipuuzia na kuona mambo ya Kimungu ni ya kiduni na watu maskini na wachini, wakati ni mambo ya msingi kuliko kitu chochote duniani,” alisema Mchungaji Simalenga.    
Naye Afisa Utumishi Mkuu wa JNIA, Bw. Priscus Mkawe alisema marehemu Swai ameacha pengo kubwa kutokana na umahiri wake katika utendaji kazi wake uliotukuka.
“Marehemu Swai alikuwa mmoja wa wafanyakazi wa kipekee aliyefanya kazi kwa bidii na kujituma na kutokana na uchapakazi wake aliwahi kuchaguliwa kuwa mfanyakazi hodari kuanzia mwaka 2001, 2003 na 2017, hivyo JNIA na TAA kwa ujumla tumempoteza mfanyakazi hodari sana,” alisema Priscus.

WATAALAM WA AFYA MOJA KUANDAA MPANGO MKAKATI WA ULINZI NA USALAMA WA VIMELEA HATARISHI

February 28, 2018

Wataalam wa Afya moja nchini ambao ni wataalam wa sekta ya Afya ya binadamu, Afya ya wanyamapori na mifugo pamoja na mazingira wameanza kuandaa Mpango Mkakati wa ulinzi na usalama wa  vimelea hatarishi utakaosaidia kuimarisha ulinzi na usalama wa sampuli za vimelea hivyo hatarishi kutoweza kueeneza  magonjwa  kwa binadamu.

Mpango huo utatoa mwongozo wa namna sekta za Afya nchini ambazo ni sekta ya Afya ya binadamu, Afya ya wanyamapori na mifugo pamoja na mazingira kushirikiana katika kuvichukua  vimelea kwa wanyama, binadamu na mimea  au  wakati wa kuvisafirisha na  kuvipeleka maabara kwa ajili ya Uchunguzi na wakati wa kuviharibu mara baada ya kuvifanyia uchunguzi.

Akiongea wakati wa Mkutano wa wataalamu wanaounda  Mtandao wa Huduma za Maabara nchini, leo tarehe 28 Februari,2018 mjini Morogoro, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bashiru Taratibu  alibainisha kuwa serikali imedhamiria kuijenga jamii yenye Afya bora kwa kuikinga na majanga yatokanayo na magonjwa ya mlipuko  hivyo imeamua kuandaa mpango huo ili kuboresha uratibu.  

Naye mratibu wa Mkutano huo anayeshughulikia masuala ya Ulinzi na Usalama wa vimelea hatarishi katika wizara ya Afya, Jacob Lusekelo, alibainisha mpango huo ambao utatoa mwongozo wa sekta za Afya kushirikiana utasaidia kupunguza maabukizi ya vimelea hivyo kwa wanyama na binadamu.

Tarehe 13 Februari 2018, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa alizindua Dawati la Uratibu la Afya moja chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, likiwa na lengo la kusimamia na kuratibu shughui za Afya moja nchini, ikiwemo wataalamu wanaounda  Mtandao wa Huduma za Maabara nchini, ambao unawajumuisha wataalamu wa kutoka katika sekta zote za afya katika masuala ya maabara.

Afya Moja ni dhana inayojumuisha sekta ya afya ya binadamu , wanyamapori, mifugo na  mazingira katika kujiandaa , kufuatilia  na kukabili magonjwa yanayoathiri binadamu ,wanyamapori na mifugo. Kwa kutambua umuhimu huo  Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, kupitia Dawati la Uratibu wa Afya moja  kwa kushirikiana na Shirika la Maabra  SANDIA na DTRA  wameandaa mkutano wataalam hao.
 Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bashiru Taratibu akieleza  jambo wakati  wa Mkutano wa wataalamu wanaounda  Mtandao wa Huduma za Maabara nchini, uliojikita katika ulinzi na usalama wa vimelea hatarishi leo tarehe 28 Februari, 2018 mjini Morogoro.
 Mtaalamu Masuala ya Mpango Mkakati  wa Maabara  kutoka Shirika la Maabara –SANDIA, Laura Jones, akifafanua umuhimu wa Mpango huo wakati  wa Mkutano wa wataalamu wanaounda  Mtandao wa Huduma za Maabara nchini, uliojikita katika ulinzi na usalama wa vimelea hatarishi leo tarehe 28 Februari, 2018 mjini Morogoro.
 Baadhi ya Wataalamu wanaounda  Mtandao wa Huduma za Maabara nchini,  wakijadiliana namna ya kuandaa  Mpango Mkakati wa ulinzi  na usalama wa  vimelea hatarishi,  leo tarehe 28 Februari, 2018 mjini Morogoro.
 Wataalamu wa Afya moja wanaounda  Mtandao wa Huduma za Maabara nchini  wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya   mkutano wa kuandaa  Mpango Mkakati wa ulinzi na usalama wa  vimelea hatarishi,  leo tarehe 28 Februari, 2018 mjini Morogoro.

CHATANDA AWAWASHIA 'MOTO' WAHANDISI WA MAJI HALMASHAURI YA MJI KOROGWE

February 28, 2018

PICHANI: Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini mkoani Tanga (CCM) Mary Chatanda (kushoto) leo Februari 28, 2018 amefika Mtaa wa Kwanduli, Kata ya Bagamoyo katika Halmashauri ya Mji Korogwe kuangalia miradi mbalimbali ikiwemo ule wa umeme kwenye vitongoji sita vya Mtaa wa Kwanduli unaotekelezwa kupitia Wakala wa Umeme Vijijini (REA). Pichani anaangalia nguzo ambapo wakati wowote zitasimikwa. (Picha na Yusuph Mussa).

Na Yusuph Mussa, Korogwe
IMMAMATUKIO

MBUNGE wa Jimbo la Korogwe Mjini Mary Chatanda amesema kitendo cha wananchi wa Kitongoji cha Kwatomokwe, Mtaa wa Kwanduli, Kata ya Bagamoyo katika Halmashauri ya Mji Korogwe mkoani Tanga kuwekewa vilula vya kuchotea maji, wakati maji hayo hayatoki, huo ni ubadhirifu wa fedha za umma.

Alisema chanzo cha kukosekana maji hayo ni kutega mabomba kwenye vyanzo vya maji ambavyo havina uhakika, ndiyo maana mradi huo uliokamilika katikati ya Januari, mwaka huu, ulitoa maji siku ya ufunguzi, lakini baada ya hapo, maji hayajatoka tena.

ZIARA YA WAZIRI MPINA KWENYE MNADA WA PUGU LEO

February 28, 2018
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Kuhaga Mpina akizungumza na wananchi katika Mnada wa Pugu, Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema.

Na Bashir Nkoromo, Pugu
Serikali ameagiza shughuli mpya za ujenzi na nyingine za maendeleo ikiwemo kilimo katika Kijiji cha Bangulo Kata ya Pugu Stesheni kusimama kuanzia leo, kusubiri mgogoro wa eneo kati ya Kijiji hicho na Mnada wa mifugo wa Pugu upatiwe ufumbuzi.

Akizungumza na wananchi leo baada ya kutembelea maeneo ya mpaka wa Mnada huo, Waziri wa Mifugo na Uvivi Luhaga Mpina ametoa agizo hilo kunusuru hali ya fukuto la mapigano katika ya wafanyabiashara kwenye mnada huo kudai Wanakijiji hicho cha Bangulo kuvamia eneo la malisho.

"Baadhi yenu mmeonyesha hapa hati za kumiliki makazi, lakini pia tunafahamu kuwa eneo la Mnada lilikuwa na ukubwa wa ekari 190, hivi sasa limebaki eneo kama asilimia 20 tu ya malisho. Hali hii inaufanya Mnada huu kukosa sifa, hivyo wakati serikali ikitafuta ufumbuzi wa kudumu naagiza shughuli zote za ujenzi na kilimo zisimame kwanza kuanzia leo," alisema Mpina.

Waziri Mpina amewataka wananchi kuishi bila hofu akisema suala lao litapatiwa ufumbuzi ambao utakuwa wa kudumu.

Habari katika Picha
 Sehemu ya eneo la Mnada wa Pugu nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, leo
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akimkaribisha kufanya ziara, Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina alipowasili kwenye Mnada wa Pugu wilayani hummo, Dar es Salaam, leo
 Waziri Mpina akimsalimia na Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo alipowasili kwenye Mnada wa Pugu leo
 Waziri Mpina akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema kabla ya kuanza ziara
 Sohia Mjema akimuongoza Waziri Mpina kwenye eneo la kufanya mazungumzo na uongozi wa Mnada huo. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dk Maria Mashungo
 Mkuu wa Mnada wa Pugu Kevamba Samwel akizungumzia hali ya maendeleo na changamoto za Mnada huo
 Matibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dk Maria Mashungo akijibu baadhi ya changamoto zilizoelezwa na mkuu wa Mnada huo
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akieleza anavyozijua na alivoanza kuzishughulia baadhi ya changamoto za Mnada huo hasa mgogoro wa arhi baina ya Mnada na Wananchi
 "Naona mda unakwenda mbio, hebu tuanze utembeleaji mipaka..." akasema waziri Mpina huku akitazama saa yake
 Waziri Mpina akijadiliana na Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema kipi waanze kati ya kuzungumza kwanza na wananchi au kukagua mipaka
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dk Maria Mashungo akiwa ameweka bakora begani wakati safari ya kukagua mipaka ikianza. Kushoto ni Katubu wa Mwenezi tawi la CCM Bangulo Kata ya Pugu Stesheni Loyce Hamisi
 Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina (kushoto) akiongoza kupanda moja ya vilima vilivyo katika Kijiji cha Bangulo wakati akikagua mipaka ya kijiji hicho na Mnada wa Pugu leo
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema naye akijiandaa kupanda kilima hicho 
 "Kwa hiyo hadi kulee ni eneo la malisho ya Mnada?" Waziri Mpina akiuliza maofisa aliofuatana nao. Wapili kushoto ni DC Mjema
 Afisa wa Mnada akimpatia maelezo waziri Mpina kuhusu lilivyo eneo la malisho ya Mnada wa Pugu 
 Kamanda wa Polisi wilaya ya Ilala Kamishna Msaidizi Salim Hamduni akiongoza msafara wakati wa kushuka baada ya Waziri Mpina kukagua badhi ya maeneo ya mipaka kati ya kijiji cha Bangulo na Mnada wa Pugu 
 Kisha waziri Mpina naye akashuka kilima hicho
 Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo (aliyenyoosha mikono) akimweleza jambo Waziri Mpina baada ya kutoka kukagua mipaka hiyo
 Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala edward Mpogolo (aliyenyoosha mikono) akimweleza jambo Waziri Mpina baada ya kutoka kukagua mipaka hiyo
 Baadhi ya nyumba katika kijiji cha Bangilo kinachodaiwa kuvamia eneo la malisho ya Mnada wa Pugu. Kushoto ni Waziri Mpina 
 "Wenyewe mpo?" Waziri Mpina akiuliza huku akichungulia kwenye geti la nyumba moja inayoonyesha kujengwa hivi karibuni ambayo inadaiwa kuwa miongoni mwa nyumba za wananchi wa kijiji cha Bangulo waliovamia eneo la malisho la Mnada wa Pugu.
 Aloyce Malya mkazi wa Kijiji cha Bangulo akizungumza wakati waziri Mpina alipozungumza na wananchi kuhusu mgogoro wa ardhi baina ya wanankijiji hicho na Mnada wa Pugu leo
 Kisha Aloyce akatia hati yake ya umiliki wa ardhi na kumkabidhi waziri Mpina
 Waziri Mpina akiipitia kwa makini hati hiyo baada ya kuipokea
 Hati yenyewe kwa karibu
 Waziri Mpina akizungumza na wananchi kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo mgogoro wa mipaka kati ya wananchi na Mnada wa Pugu
 Wananchi wakimsikiliza waziri Mpina 
 Waziri Mpina akiwaaga baada ya mazungumzo. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO