Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt.
Augustine Mahiga akizungumza na Balozi wa Vietnam nchini, Mhe.
Kim Nguyen Doanh. Katika mazungumzo yao walisisitiza umuhimu wa
kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizi mbili hususan katika masuala ya
biashara na uwekezaji.
|
Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Justa Nyange (kushoto)
pamoja na Bw. Emmanuel Luangisa (katikati), Afisa Mambo ya Nje na Bw.
Magabilo Murobi (kulia), Katibu wa Waziri wakifuatilia mazungumzo kati
ya Mhe. Mahiga na Mhe. Kim Nguyen Doanh (hawapo pichani) |
…..Mkutano wa Waziri Mahiga na Balozi wa Japan
|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Balozi wa Japan nchini, Mhe.
Masaharu Yoshida. Mazungumzo yao yalijikita kwenye kuimarisha
ushirikiano katika masuala mbalimbali ya manufaa kwa nchi hizi mbili. |
|
Mkurugenzi
wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Celestine Mushy akifafanua jambo
wakati wa mazungumzo kati ya Mhe. Mahiga na Balozi wa Japan nchini,
Mhe. Yoshida (hawapo pichani). Wengine katika picha ni Kaimu Mkurugenzi
wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Justa Nyange (kushoto)
Bw. Abdallah Kirungu (katikati), Afisa Mambo ya Nje na Bw. Magabilo Murobi (kulia), Katibu wa Waziri. |
Share this