MKUU wa wilaya ya Tanga ,Thobias Mwilapwa kulia akimkabidhi Kombe la Ubingwa wa Mashindano ya Rede Nahodha wa timu ya Magomeni Sisters
Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa kulia akimkabidhi kombe mshindi wa
pili ambao ni Mkwakwani Baisket
Mabingwa wa Mashindano ya Rede ambao ni timu ya Magomeni Sisters wakiwa na kombe lao mara baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa
Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akizungumza wakati akifunga mashindano hayo yaliyofanyika kwenye viwanja vya CCM Mkwakwani mjini Tanga
Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa kulia akimkabidhi Cheti cha kutambua mchango wake katika mashindano hayo Dj
Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa kulia akimkabidhi Cheti cha kutambua mchango wake katika mashindano hayo Dj Bad Fuvu
Sehemu ya Majaji wa Mashindano hayo wakiwa kazini
Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa wa pili kutoka kulia akiwa na Muandaaji wa mashindano ya Rede Nassoro Makau kushoto kutoka ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Five kulia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga Faidha Salim
Timu ya Magomeni Sisters wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa na wageni wengine wakiwemo waaandaaji wa mashindano hayo
Sehemu ya timu ambazo zilikuwa zikishiriki mashindano hayo wakiwa na mashabiki wakifuatilia mechi ya fainali
MKUU wa wilaya
ya Tanga Thobias Mwilapwa ameipongeza Kampuni ya Five Brothers kwa kuonyesha
ubinifu mkubwa kuanzisha mashindano ya mchezo wa rede ambayo imesaidia kurudisha
michezo ya zamani iliyokuwa ikipendwa.
Pongezi hizo
zilitolewa mwishoni mwa wiki wakati akifunga fainali za mashindano hayo ambapo
mshindi wa kwanza alikuwa ni timu ya Magomeni Sisters ambao walizawadiwa fedha
taslimu 120,000 kikombe cha mashindano hayo, medali, unga wa ngano kilo 25 na
mafuta lita 10.
Huku mshindi wa
pili ambao ni Mkwakwani Baisket iliweza kupata kitita cha
sh.70,000,medali,ngano kg 5 na mafuta lita 5 ambazo zilitolewa na mgeni rasmi
katika mashindano hayo.
Alisema kimsingi
uanzishwaji wa mashindano hayo umekuwa ni chachu kubwa kuweza kujenga umoja na
mshikamano kwa vijana kuweza kutumia michezo kama sehemu ya kuimarisha miili
yao na kujiepusha na vitendo viovu kwenye jamii.
“Ubunifu huu
ambao ulionyesha wakati wa michuano hii ya rede ni mzuri na unapaswa
kuendelezwa kila mwaka na sisi tutaendelea kuwaunga mkono kwa kuhakikisha
yanafanyika kwa waledi mkubwa “Alisema.
Awali
akizungumza, Mratibu wa Mashindano hayo kutoka Kampuni ya Five Brothers,Nassoro
Makau alisema mchezo wa rede ni miongoni mwa michezo ambayo ilikuwa
imesahaulika kwa kipindi kirefu hivyo wakaona wairudishe ili kuweza kuinua
vipaji vinavyopatikana kupitia mchezo huo.
“Kwa kweli sisi
kama Kampuni ya Five Brothers tumeona na kudhamiria kwa dhati kuona namna ya
kurudisha michezo ya asili ambayo ni
pendwa kwa mkoa wa Tanga kwa kuipa thamani kwani mchezo kama ukuti ukuti na
rede ni michezo ya asili hivyo tunapoirudisha tunasaidia kurudisha enzi na
kuwakumbusha watu mambo mengi “Alisema Makau.
Alisema msimu
huu mashindano hayo yalianza February 8 mwaka huu kwa mtindo wa ligi kwa
kushirikisha timu 11 za jiji la Tanga na yamesaidia vijana kushiriki kwa
kuonyesha vipaji vyao.
Naye kwa upande
wake,Mwenyekiti wa Kongamano la Vijana na Balozi wa Vijana Mkoa wa
Tanga,Selemani Mssey alisema mchezo huo utasaidia kuondoa vitendo vya umbea na
kusutana kwa wasichana.
“Tanga wasichana
walikuwa wakiongoza kusuta lakini uanzishwaji wa mashindano hayo utasaidia
kuondoa hali hiyo pia kutoa fursa kwao kutumia michezo kama sehemu ya
kuimarisha miili yao lakini kupata kipato “Alisema.