Wataalam
wa Afya moja nchini ambao ni wataalam wa sekta ya Afya ya binadamu,
Afya ya wanyamapori na mifugo pamoja na mazingira wameanza kuandaa
Mpango Mkakati wa ulinzi na usalama wa vimelea hatarishi utakaosaidia
kuimarisha ulinzi na usalama wa sampuli za vimelea hivyo hatarishi
kutoweza kueeneza magonjwa kwa binadamu.
Mpango
huo utatoa mwongozo wa namna sekta za Afya nchini ambazo ni sekta ya
Afya ya binadamu, Afya ya wanyamapori na mifugo pamoja na mazingira
kushirikiana katika kuvichukua vimelea kwa wanyama, binadamu na mimea
au wakati wa kuvisafirisha na kuvipeleka maabara kwa ajili ya
Uchunguzi na wakati wa kuviharibu mara baada ya kuvifanyia uchunguzi.
Akiongea
wakati wa Mkutano wa wataalamu wanaounda Mtandao wa Huduma za Maabara
nchini, leo tarehe 28 Februari,2018 mjini Morogoro, Kaimu Mkurugenzi
Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bashiru Taratibu
alibainisha kuwa serikali imedhamiria kuijenga jamii yenye Afya bora kwa
kuikinga na majanga yatokanayo na magonjwa ya mlipuko hivyo imeamua
kuandaa mpango huo ili kuboresha uratibu.
Naye
mratibu wa Mkutano huo anayeshughulikia masuala ya Ulinzi na Usalama wa
vimelea hatarishi katika wizara ya Afya, Jacob Lusekelo, alibainisha
mpango huo ambao utatoa mwongozo wa sekta za Afya kushirikiana utasaidia
kupunguza maabukizi ya vimelea hivyo kwa wanyama na binadamu.
Tarehe
13 Februari 2018, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Kassim Majaliwa alizindua Dawati la Uratibu la Afya moja chini ya Ofisi
ya Waziri Mkuu, likiwa na lengo la kusimamia na kuratibu shughui za Afya
moja nchini, ikiwemo wataalamu wanaounda Mtandao wa Huduma za Maabara
nchini, ambao unawajumuisha wataalamu wa kutoka katika sekta zote za
afya katika masuala ya maabara.
Afya
Moja ni dhana inayojumuisha sekta ya afya ya binadamu , wanyamapori,
mifugo na mazingira katika kujiandaa , kufuatilia na kukabili magonjwa
yanayoathiri binadamu ,wanyamapori na mifugo. Kwa kutambua umuhimu huo
Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, kupitia Dawati la Uratibu
wa Afya moja kwa kushirikiana na Shirika la Maabra SANDIA na DTRA
wameandaa mkutano wataalam hao.
Kaimu
Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bashiru
Taratibu akieleza jambo wakati wa Mkutano wa wataalamu wanaounda
Mtandao wa Huduma za Maabara nchini, uliojikita katika ulinzi na usalama
wa vimelea hatarishi leo tarehe 28 Februari, 2018 mjini Morogoro.
Mtaalamu
Masuala ya Mpango Mkakati wa Maabara kutoka Shirika la Maabara
–SANDIA, Laura Jones, akifafanua umuhimu wa Mpango huo wakati wa
Mkutano wa wataalamu wanaounda Mtandao wa Huduma za Maabara nchini,
uliojikita katika ulinzi na usalama wa vimelea hatarishi leo tarehe 28
Februari, 2018 mjini Morogoro.
Baadhi
ya Wataalamu wanaounda Mtandao wa Huduma za Maabara nchini,
wakijadiliana namna ya kuandaa Mpango Mkakati wa ulinzi na usalama wa
vimelea hatarishi, leo tarehe 28 Februari, 2018 mjini Morogoro.
Wataalamu
wa Afya moja wanaounda Mtandao wa Huduma za Maabara nchini wakiwa
katika picha ya pamoja mara baada ya mkutano wa kuandaa Mpango
Mkakati wa ulinzi na usalama wa vimelea hatarishi, leo tarehe 28
Februari, 2018 mjini Morogoro.