WAVUVI WAASWA KUZINGATIA SHERIA,TARATIBU ZA UVUVI KUZILINDA RASILIMALI ZIWA VICTORIA

January 27, 2018
NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega ameteketeza Nyavu haramu 242 zenye thamani ya Sh Mil.242 baada ya wavuvi kuzisalimisha wenyewe katika kisiwa cha Zilagula kilichopo halmshauri ya Buchosa wilayni Sengerema mkoani Mwanza.

Akizungumza wakati wa uteketezaji wa nyavu hizo, Ulega aliwapongeza wavuvi hao kwa hatua hiyo walioichukua huku akikazia msimamo wa serikali wa kupambana na uvuvi halamu. Pamoja na kuwapongeza huko,Ulega aliwasisitiza wavuvi hao kuzingatia sheria na taratibu za uvuvi ili kuzilinda rasilimali hiyo, ambayo ilikuwa inaelekea kutoweka.

"Kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa samaki, wazazi walikuwa wamebaki asilimia nne, wenye hadhi ya kuvuliwa kwa maana ya sentimita 50 hadi 85 wamebaki asilimia tatu na wachanga wamebaki asilimia 93, na kama uvuvi huu ungeendelea maana yake ziwa lingebaki jangwa," alisema Ulega

Waziri Ulega aliwataka wavuvi hao kununua nyavu zinazokubalika kwenye viwanda ambavyo vinauza nyavu hizo,  badala ya kuendelea kutumia nyavu zisizoruhusiwa kwani watapata hasara kwa kuteketezewa na wengine kushtakiwa kwa mujibu wa sheria.

kwa upande wake kiongozi kazi maalumu mkoa wa kioparesheni Sengerema, Charles Lwekaza alisema baada ya kufanya operesheni hiyo iliyoanza mapema Januari mwaka huu, baadhi ya wavuvi waliamua kuzisalimisha nyavu hizo wenyewe bila shuruti. 


kwa upande wake kiongozi kazi maalumu mkoa wa kioparesheni Sengerema, Charles Lwekaza alisema baada ya kufanya operesheni hiyo iliyoanza mapema Januari mwaka huu baadhi us wavuvi waliamua kusalimisha nyavu  hizo wenyewe bila shuruti.

Alisema nyavu zinazokubalika kwa mujibu wa sheria, nyavu za dagaa zinatakiwa ziwe na milimita 8, nyavu za sangara inchi 6 hadi tisa na ndoano za sato inatakiwa zenyewe ziwe namba 4, hadi 12, hizi ndio zana sahihi zinazotakiwa kuonekana ziwani," alisema Lwekaza

Naye Benzi Nestory ambaye nimmoja wa wavuvi aliomba kupata muongozo wa sehemu sahihi ya kupata zana hizo haramu kwa haraka badala ya kuambiwa kwa mdomo kuwa nyavu hizo zinapatikana ili kuondokana na hasara wanazopata.

Kwa upande wake Joel Lusigwa alilalamikia upande wa faini Sh700000 kuwa kubwa wanayotozwa pindi wanapokutwa na kosa hivyo kuomba wapunguziwe ikilinganishwa na maeneo mengine ambayo wanatozwa faini kidogo. Hata hivyo waziri Ulega alisema licha ya kuwapo sheria nyingine zinazowakandamiza wavuvi lakini alisema faini hiyo ya Sh700000 ni pamoja faini ya kutokuwa na leseni na usajili ambayo ni Sh .200000 huku faini ya kuharibu mazingira ndani yaziwa ikiwa ni Sh .500000 ambazo hazitabadilishwa lengo ni kumtia uchungu mtuhumiwa.
 Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega  akiongoza shughuli za kuteketeza Nyavu haramu 242 zenye thamani ya Sh Mil.242  baada ya wavuvi kuzisalimisha wenyewe katika kisiwa cha Zilagula  kilichopo halmshauri ya Buchosa wilayani Sengerema mkoani Mwanza
 .Wavuvi wakisogeza  Nyavu haramu 242 zenye thamani ya Sh Mil.242  eneo la kuchomea  baada ya kuzisalimisha wenyewe katika kisiwa cha Zilagula  kilichopo halmshauri ya Buchosa wilayani Sengerema mkoani Mwanza.
 Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizungumza na wavuvi  katika kisiwa cha Zilagula  kilichopo halmshauri ya Buchosa wilayani Sengerema mkoani Mwanza.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »