MAAMUZI YA KAMATI YA BODI YA LIGI KUU YA UENDESHAJI NA
USIMAMIZI WA LIGI KILICHOFANYIKA JANUARI 25, 2018 OFISI ZA TFF, UWANJA
WA KUMBUKUMBU YA KARUME- DAR ES SALAAM
LIGI KUU YA VODACOM
Mechi
namba 95 (Mbeya City 1 vs Kagera Sugar 1). Klabu ya Mbeya City imepigwa
faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa kutumia mlango usio rasmi kuingia
uwanjani katika mechi hiyo iliyofanyika Januari 1, 2018 jijini Mbeya,
kitendo ambacho ni kinyume na Kanuni ya 14(14) ya Ligi Kuu kuhusu
Taratibu za Mchezo. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya
14(49) ya Ligi Kuu.
Kamati
iliiagiza Sekretarieti ya Bodi ya Ligi kutoa waraka kwa wamiliki wa
viwanja kuhakikisha timu zinaingia uwanjani kwa kutumia milango rasmi
tu.
Mechi
namba 100 (Tanzania Prisons 3 vs Mbeya City 2). Kocha wa Mbeya City,
Ramadhani Mwazurimo amefungiwa mechi mbili na kupigwa faini ya sh.
500,000 (laki tano), adhabu ambayo imezingatia Kanuni ya 40(11) ya Ligi
Kuu kuhusu Udhibiti wa Makocha.
Kocha
Mwazurimo aliondolewa kwenye benchi (ordered off) na Mwamuzi baada ya
kumtolea lugha ya kashfa katika mechi hiyo iliyochezwa Januari 14, 2018
kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
Pia
klabu ya Mbeya City imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana
na washabiki wake kuingia uwanjani na kumzonga mwamuzi kwa madai
alikataa kutoa penalti kwa timu hiyo. Adhabu hiyo imetolewa kwa
kuzingatia Kanuni ya 42(1) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Klabu.
Kamati
imeteua wajumbe watatu kupitia mkanda wa mechi hiyo ambapo pamoja na
mambo mengine itachunguza kiwango cha uchezeshaji cha Mwamuzi wa mechi
hiyo, Bw. Israel Nkongo na kuwasilisha taarifa yake kwa ajili ya hatua
zaidi.
Mechi
namba 103 (Majimaji 1 vs Azam 1). Klabu ya Azam FC imepigwa faini ya
sh. 500,000 (laki tano) kutokana na kukataa wachezaji wake wakaguliwe
ndani kwa madai kuwa chumba kimepuliziwa dawa katika mechi hiyo
iliyofanyika Januari 18, 2018 Uwanja wa Majimaji mjini Songea.
Kitendo
cha timu hiyo ni kinyume na Kanuni ya 14(13) ya Ligi Kuu kuhusu
Taratibu za Mchezo, na adhabu dhidi yao imezingatia Kanuni ya 14(49) ya
Ligi Kuu. Pia klabu hiyo imeandikiwa barua ya kutakiwa kuthibitisha
madai yake kuwa chumba hicho kilikuwa kimepuliziwa dawa.
Mechi
namba 104 (Simba 4 vs Singida United 0).Mtunza Vifaa wa Singida United
FC, Mussa Rajab amefungiwa mwezi mmoja na kupigwa faini ya sh. 300,000
(laki tatu) kutokana na kuingia uwanjani baada ya filimbi ya mapumziko
na kumlalamikia mwamuzi.
Kitendo
alichofanya Mtunza Vifaa huyo katika mechi hiyo iliyochezwa Januari 18,
2018 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kimekiuka Kanuni ya
14(10) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo. Adhabu hiyo ni uzingativu
wa Kanuni ya 41(2) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Viongozi.
Mechi
namba 106 (Mbao 0 vs Stand United 1). Klabu ya Stand United imepewa
Onyo Kali kutokana na timu yake kuchelewa kwenye kikao cha maandalizi ya
mechi (pre match meeting) kwa dakika sita, na pia kuchelewa kuingia
uwanjani kwa dakika tisa katika mechi hiyo iliyofanyika Januari 20, 2018
Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Adhabu
kwa klabu hiyo iliyokiuka Kanuni ya 14(2a) ya Ligi Kuu, imetolewa kwa
kuzingatia Kanuni ya 14(3) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.
Mechi
namba 112 (Kagera Sugar 0 vs Simba 2). Suala la mchezaji wa Kagera
Sugar, Juma Nyoso kumpiga shabiki baada ya mechi hiyo iliyochezwa
Januari 22, 2018 Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba kumalizika, limepelekwa
Kamati ya Nidhamu ya TFF kwa ajili ya hatua za kinidhamu.
LIGI DARAJA LA KWANZA
Mechi
namba 44 Kundi A (African Lyon 2 v Friends Rangers 1). Mchezaji Almasi
Mkinda wa Friends Rangers amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh.
300,000 (laki tatu) baada ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kumpiga
ngumi mchezaji wa African Lyon katika mechi hiyo iliyofanyika Januari
14, 2018 Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Adhabu hiyo ni kwa mujibu
wa Kanuni ya 37(3) ya Daraja la Kwanza kuhusu Udhibiti wa Wachezaji.
Nao
wachezaji Mtoro Hamisi wa Friends Rangers, na Prosper Mushi wa African
Lyon wamefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 300,000 (laki tatu)
kila mmoja baada ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kupigana
uwanjani. Adhabu imezingatia Kanuni ya 37(3) ya Ligi Daraja la Kwanza
kuhusu Udhibiti wa Wachezaji.
Daktari
wa Friends Rangers, Rajabu Shabani amefungiwa miezi mitatu na kupigwa
faini ya sh. 200,000 (laki mbili) kwa kuwatolea lugha ya matusi na
dharau waamuzi wa mechi hiyo. Adhabu imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya
41(2) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Udhibiti wa Viongozi.
Klabu
ya African Lyon imepigwa faini ya sh. 300,000 (laki tatu) baada ya
kuonyeshwa kadi zaidi ya tano katika mechi hiyo. Adhabu hiyo imezingatia
Kanuni ya 42(10) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Udhibiti wa Klabu.
Mechi
namba 45 Kundi A (JKT Tanzania 5 v African Lyon 1). Klabu ya African
Lyon imepigwa faini ya sh. 300,000 (laki tatu) kwa kukiuka Kanuni ya
14(13) kutokana na kugoma kuingia vyumbani katika mechi hiyo iliyochezwa
Januari 20, 2018 kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo ulioko Mbweni
jijini Dar es Salaam. Adhabu dhidi ya klabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni
ya 14(49) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Taratibu za Mchezo.
Nayo
JKT Tanzania imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na
washabiki wake kuingia eneo la kuchezea kushangilia ushindi. Klabu hiyo
imeadhibiwa kwa mujibu wa Kanuni ya 42(1) ya Ligi Daraja la Kwanza
kuhusu Udhibiti wa Klabu.
Mechi
namba 41 Kundi B (JKT Mlale 1 v Mawenzi Market 0). Daktari wa Mawenzi,
Novatus Ngowi amepelekwa Kamati ya Nidhamu ya TFF baada ya kuwatolea
waamuzi lugha isiyokuwa ya kiungwana katika mechi hiyo iliyofanyika
Januari 13, 2018 kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea.
Mechi
namba 43 Kundi B (Mbeya Kwanza 0 vs KMC 0). Kocha wa Mbeya Kwanza, Maka
Mwalwisi amepelekwa Kamati ya Nidhamu ya TFF kwa kuzungumza na
waandishi wa habari baada ya mechi hiyo iliyochezwa Januari 13, 2018
Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya kumalizika akiwashambulia
viongozi wa TFF akidai wanaandaa timu za kupanda Ligi Kuu, ndiyo maana
waamuzi wananyonga haki yao ya kupata ushindi.
Mechi
namba 47 Kundi B (Polisi Tanzania 0 vs Coastal Union 0). Klabu ya
Polisi Tanzania imepigwa faini ya jumla ya sh. 1,000,000 (milioni moja)
kutokana na gari la washabiki wa timu hiyo kuingia uwanjani, na
kuzunguka uwanja wakati timu zikifanya mazoezi. Pia wakati wa mapumziko
na baada ya mchezo kumalizika washabiki wa timu hiyo waliwafuata waamuzi
na kutaka kuwapiga.
Vilevile
washabiki wa timu hiyo walitoa lugha chafu kwa viongozi wa Chama cha
Mpira wa Miguu Mkoa wa Kilimanjaro (KRFA) katika mechi hiyo iliyochezwa
Januari 20, 2018 Uwanja wa Ushirika mjini Moshi. Adhabu hiyo imetolewa
kwa kuzingatia Kanuni ya 42(1) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Udhibiti
wa Klabu.
Mechi
namba 44 Kundi C (Biashara United 2 vs Alliance Schools 0). Klabu ya
Alliance Schools imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na
timu yake kutoingia vyumbani katika mechi hiyo iliyofanyika Januari 13,
2018 katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma. Adhabu hiyo ni
kwa mujibu wa Kanuni ya 14(49) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Taratibu
za Mchezo.
Mechi
namba 45 Kundi C (JKT Oljoro 1 vs Dodoma FC 1). Mwamuzi Msaidizi Namba
Moja, Emmanuel Muga na Mwamuzi wa Akiba, Gilbyrth Mrina wamepata alama
za chini hivyo kukosa sifa ya kuendelea kuchezesha Ligi.
Hivyo,
Kamati imeteua wajumbe watatu kupitia mkanda wa mechi hiyo ambapo
pamoja na mambo mengine itachunguza kiwango cha uchezeshaji cha waamuzi
kabla ya kuchukuliwa hatua zaidi dhidi yao.
Mechi
namba 47 Kundi C (Biashara United 1 vs Rhino Rangers 1). Daktari wa
Viungo wa Rhino Rangers, Ahamad Mgongo na kipa Mohamed Ibrahim Salumu wa
Rhino Rangers wamesimamishwa hadi suala lao la utovu wa nidhamu
waliofanya litakaposikilizwa na Kamati ya Nidhamu ya TFF. Wamesimamishwa
kwa mujibu wa Kanuni ya 9(5) ya Ligi Daraja la Kwanza.
Mbali
ya kumpiga teke Msimamizi Msaidizi wa Kituo cha Mara, Mgongo pia wakati
vurugu zikiendelea katika mechi hiyo iliyofanyika Januari 21, 2018
Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma alimchapa kibao Mwamuzi
Msaidizi Namba Moja, Athuman Rajabu.
Naye
kipa Salumu baada ya kumuangusha kwa makusudi ndani ya eneo la hatari
mchezaji wa Biashara United, na refa kuamuru adhabu ya penalti dhidi
yake alimpiga ngumi kwa makusudi mchezaji huyo wa Biashara United. Baada
ya vurugu kutulia Mwamuzi alimuonyesha kadi nyekundu. Lakini Kipa huyo
baada ya kuamuliwa kutoka nje alimpiga Mwamuzi ngumi ya kisogoni.
Mechi
namba 48 Kundi C (Transit Camp 0 vs Alliance Schools 3). Wachezaji
Mohamed Suleiman Ussi, Khalid Mahmud Konobile, Abubakar Ramadhan na
Victor William Alimwene wa Transit Camp wamepelekwa Kamati ya Nidhamu ya
TFF kwa kumkimbilia Mwamuzi baada ya mechi kumalizika kwa lengo la
kumfanyia vurugu kabla ya askari polisi kuingilia kati.
Walifanya kitendo hicho katika mechi hiyo iliyochezwa Januari 21, 2018 kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
LIGI DARAJA LA PILI
Mechi namba 21 Kundi C (The Mighty Elephant 2 v Burkina Faso 2).
Mchezaji
Gideon Joram Richard wa The Mighty Elephant anapelekwa Kamati ya
Nidhamu ya TFF kwa kitendo chake cha kwenda karibu na chumba cha waamuzi
baada ya mechi na kuwakashfu kuwa ni mabwege katika mchezo huo
uliofanyika Januari 15, 2018 Uwanja wa Majimaji mjini Songea.
AJENDA 62/MSC/2018- MALALAMIKO YA DODOMA FC
Kamati
imesikiliza malalamiko ya timu ya Dodoma FC dhidi ya JKT Oljoro katika
mechi yao iliyochezwa Januari 21, 2018 kwenye Uwanja wa Ushirika mjini
Moshi. Malalamiko hayo yalikuwa na sehemu mbili; moja ni uhalali wa
mchezaji wa JKT Oljoro, Haki Rubea kuwa hakuwa na leseni, na mbili ni
kudai kuwa Mwamuzi na Mwamuzi Msaidizi Namba Moja walikataa bao lao
halali.
Baada
ya kupitia malalamiko hayo, Kamati imebaini kuwa Haki Rubea ni mchezaji
wa JKT Oljoro mwenye leseni namba 961111011 iliyotolewa na Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), hivyo ni mchezaji halali (qualified
player). Vilevile Kamati haina mamlaka ya kukubali bao ambalo
limekataliwa na Mwamuzi uwanjani. Hivyo, Kamati imetupa malalamiko ya
Dodoma FC kwa hoja zote mbili.
Hata
hivyo, Kamati imejiridhisha kuwa Kamishna wa mechi hiyo Paul Opiyo na
Mwamuzi wa Akiba, Gilbyrth Mrina walifanya makosa kumruhusu mchezaji
huyo kucheza bila kuonyesha leseni yake, kitendo ambacho ni kinyume na
Kanuni ya 14(16) na 14(17) za Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Taratibu za
Mchezo.
Kamati
imeteua wajumbe watatu kupitia mkanda wa mechi hiyo ambapo pamoja na
mambo mengine itachunguza kiwango cha uchezeshaji cha Mwamuzi Msaidizi
Namba Moja, Emmanuel Muga na Mwamuzi wa Akiba, Gilbyrth Mrina na
kuwasilisha taarifa yake kwa ajili ya hatua Zaidi.