SERIKALI YAMPA MWEZI MMOJA MKANDARASI KUMALIZIA MAJENGO YA CHUO.

January 27, 2018
Mshauri elekezi wa mradi wa upanuzi na ujenzi katika Chuo Cha Uuguzi Mtwara NTC na Chuo Cha Maafisa Tabibu Mtwara CoTc Arch. Benjamini Kasiga aliyevaa fulana ya bluu akiwakilisha mada katika kikao kifupi kilichofanyika chuoni hapo wakati wa ukaguzi wa majengo ya chuo hiko uliofanywa na jopo la Wakaguzi kutoka Wizara ya Afya Mkoani Mtwara.
Mkandarasi kutoka kampuni ya Ujenzi na Uhandisiz Nandhra wa kwanza kushoto akiwapa maelezo baadi ya wakaguzi wa jengo hilo kutoka Wizara ya Afya wakati wa ukaguzi wa majengo ya Chuo Cha Uuguzi Mtwara na Chuo Cha Maafisa Tabibu Mtwara CoTc uliofanyika leo mkoani humo. 
aimu Mkurugenzi wa kitengo cha kusanifu Majengo Wizara ya Afya Arch. Daniel Mwakasungura aliyevaa shati jekundu akiangalia moja ya sehemu ya jengo la Chuo Cha Uuguzi Mtwara NTC na Chuo Cha Maafisa Tabibu Mtwara CoTc wakati wa ukaguzi wa majengo ya chuo hiko uliofanyika leo mkoani humo, katikati ni Mratibu wa ujenzi huo Dkt. Joachim Catherine na kulia ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi Wizara ya Afya Bw. Castro Simba.
engo la wagonjwa Kutoka nje la Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini ambalo lipo kwenye ujenzi bado ambapo limegharimu kiasi cha shilingi Bilioni 1. 7 za Kitanzania na lengo la ujenzi wa Hospitali hiyoni kuweza kutoa huduma za kibingwa.Picha Na Wizara ya Afya-MTWARA
Baadhi ya Majengo ya Chuo Cha Uuguzi Mtwara NTC Chuo Cha Maafisa Tabibu Mtwara na CoTc yakiwa yamekamilika katika mradi wa ujenzi wa Ujenzi,Upanuzi na ukarabati wa majengo ya chuo hiko na Chuo Cha maafisa Tabibu mtwara yalipokaguliwa na wakaguzi wa jengo hilo kutoka Wizara ya Afya leo mkoani Humo.
NA WAMJW-MTWARA

SERIKALI Kupitia Wizara ya Afya imeagiza Kampuni ya Ujenzi na Uhandisi Nadhra kumalizia kazi ya kurekebisha kasoro zilizotokana na ujenzi katika majengo ya Chuo Cha Uuguzi Mtwara ( NTC) na Chuo cha Maafisa Tabibu mkoani humo (COTC) ili kuweza kudahili wanafunzi wengi zaidi.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Ununuzi na Ugavi Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Castro Simba wakati wa ukaguzi wa majengo hayo mkoani Mtwara.

“Majengo haya yalimalizika Desemba 2016 tukatoa kipindi cha mwaka mmoja kujiridhisha na ubora wake lakini kuna baadhi ya maeneo hayajakidhi ubora hivyo mkandarasi anatakiwa kurekebisha ndani ya mwezi mmoja” alisema Bw. Simba.

Aidha Bw. Simba amesema kuwa mradi huo wa kupanua, kukarabati na kujenga majengo hayo yanafanyika katika vyuo vitano nchini ikiwemo Hospitali ya Kairuki Dar es salaam, Bagamoyo, Chuo cha Uuguzi Mtwara (NTC), Chuo Cha Maafisa Tabibu (CoTC) na Chuo cha St. Bakhita cha Sumbawanga.

Kwa upande wake Mratibu wa Kuimarisha Mifumo ya Afya na Mratibu wa Mradi huo kutoka Wizara ya Afya Dkt. Joachim Catherine amesema kuwa mradi huo uliofadhiliwa na Global Fund umehusisha ujenzi Wa mabweni matatu yenye vyumba 120, Nyumba za watumishi nane katika chuo cha maafisa tabibu. Katika na Chuo cha uuguzi Mtwara.

Aidha Dkt. Catherine amesema kuwa Miradi yote imegharimu kiasi cha Shilingi bilioni 3.3 za kitanzania na kulifanyika ukarabati na upanuzi Wa madarasa, ofisi za wakufunzi, maktaba pamoja na maabara za vitendo.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo Cha Uuguzi Mtwara (NTC) Bw. Frolian Mbungu amesema kuwa amefurahishwa na ukaguzi huo kwani utamfanya apokee majengo kwa kujiamini na kuyatumia kwa ufasaha.

Aidha wakaguzi hao kutoka Wizara ya Afya wakiongozwa na Mkurugenzi wa Sera na Mipango Dkt. Edward Mbanga walitembelea jengo la wagonjwa Kutoka nje la Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini ambalo limegharimu kiasi cha shilingi Bilioni 1. 7 za Kitanzania na lengo la ujenzi wa Hospitali hiyo ni kuweza kutoa huduma za kibingwa.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »