NAIBU WAZIRI WA MADINI BITEKO ,AMEWATAKA WACHIMBAJI WADOGO KUZINGATIA SHERIA YA USALAMA KWENYE MAENEO YAO YA KAZI

January 14, 2018
Naibu waziri wa madini Doto Biteko,Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Buntumbili  Wilayani Bukombe ambapo kulitokea tukio la mchimbaji kufukiwa na kifusi wakati alipokuwa kwenye shughuli za uchimbaji.
Naibu waziri wa madini Doto Biteko,akisaini kwenye kitabu cha wageni wakati alipokuwa akiwasili kwenye ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Geita. 
Afisa madini wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Ally Maganga akitoa taarifa ya shughuli za madini mbele ya Naibu waziri wa madini Doto Biteko .
Naibu waziri wa madini Doto Biteko Akizungumza na Viongozi na Watendaji mbalimbali ngazi ya Mkoa wakati wa ziara yake ya kikazi.
Naibu waziri wa madini Doto Biteko   pamoja na viongozi wa Wilaya ya Bukombe wakiwa kwenye eneo ambalo ajali ya mchimbaji kufukiwa na kifusi ilitokea 
Baadhi ya viongozi na Naibu waziri wa madini Doto Biteko wakiwa kwenye shimo ambalo ndipo mchimbaji mdogo ambaye alipoteza uhai wakati akiwa kwenye shughuli za uchimbaji.
Naibu waziri wa madini Doto Biteko akipatiwa maelezo ya namna ajali hiyo ilivyotokea mgodini hapo.
Mmiliki wa mgodi huo,akitoa maelezo kwa Naibu waziri wa madini   namna ambavyo wachimbaji hao walivyovyamia eneo hilo na kuanza shughuli za uchimbaji hali ambayo imesababisha mmoja wao kufukiwa na kifusi.

Naibu waziri wa madini Doto Biteko  akitoa mkono wa pole kwa familia ambayo imekumbwa na msiba wa kuondokewa na kijana wao ambaye alifukiwa na kifusi wakati akiwa kwenye kazi ya uchimbaji.

Naibu waziri wa madini ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe,Doto Biteko akisalimiana na kutoa pole kwa kaka yake na marehemu wakati alipofika nyumbani kwao na marehemu.(PICHA NA JOEL MADUKA)
 
Naibu waziri wa madini ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe,Doto Biteko akifurahia na wananchi wa kijiji cha Ikalanga wakati alipokwenda kuzungumza nao juu ya mikakati ya maendeleo.
Na,Joel Maduka,Geita.

Naibu waziri wa madini Doto Biteko amewataka wachimbaji ambao
wanamiliki leseni kuhakikisha wanazingatia sheria  ambazo wamepewa likiwemo suala la kuweka
mazingira mazuri ya utendaji  kazi kwenye
maeneo yao ya mgodi ili kuepukana na  majanga
ambayo yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara kwenye shughuli za uchimbaji.
Akizungumza wakati alipotembelea na kutoa pole kwenye  mgodi mdogokijiji cha Buntubili  eneo ambalo hivi
karibuni mchimbaji mmoja aliangukiwa na kifusi na kufariki.
Naibu waziri Doto alisema ni vyema kwa kila mwenye leseni
kuhakikisha usalama unakuwa ni jambo la kwanza  huku akimwagiza afisa madini kufuatilia migodi
yote kama imewekwa mabango ambayo yanaelekezea suala la usalama kwenye
mazingira hayo.
“Hatutaki kuona hata mtanzania mmoja
anakufa katika  mazingira ya uzembe tunatamani
tuone  watanzania wote wanachimba
wanaendeleza mali na wanabaki kuwa salama kwaajili ya kulihudumia Taifa hili
,Taifa hili linawaitaji watu wote kwa hiyo nitoe wito kila mwenye leseni maali
popote alipo ahakikisha kwamba mazingira yake ya kazi usalama kiwe kipaumbele
na sasa kuanzia leo afisa madini ninakuagiza wote wenye leseni ambao
wanaendeleza migodi waweke mabango yanayoeleza umuhimu wa usalama kila kwenye
mgodi unaofanya kazi”Alisisitiza Mh,Doto.
 
Pamoja na hayo Naibu Waziri wa Madini
amewataka
wananchi kutokuingia kwenye maeneo ambayo yamesimamishwa na  ambayo ni hatarishi kwani kufanya hivyo wanaweza
kujisabasha hatari ya kupoteza maisha  kutokana na maeneo hayo kutokuwa kwenye hali
nzuri ya uchimbaji.
Akisoma taarifa kwa Naibu waziri wa madini,mlinzi wa eneo hilo
la mgodi ,Bw Christopha Mazige .amesema kuwa ajali hiyo ilitokana na ubishi wa
vijana watatu ambao walivamia mgodini hapo kwa lengo la kutafuta mali lakini
ghafla  wakiwa kwenye mabishano sehemu
moja ya ardhi alipokuwa amesimama kijana ambaye alifukiwa na kifusi ilikatika
na kushuka naye kwenye shimo kutokana na hali hiyo wenzake walikimbia.
Kwa upande wake Afisa Madini Mkazi Mhandisi Ally Maganga amesema
bado kuna changamoto zinazoikabili Sekta ya madini kama baadhi ya Wachimbaji wadogo
kushindwa kulipa kwa wakati tozo stahiki za madini kama vile ada za mwaka za
leseni na Mrabaha wa madini.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »