Mke
wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akizungumza katika mahafali ya
kwanza ya Shule ya Awali na Msingi ya Wonder Kids ya Mini Ruangwa,
Desemba 2, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mke
wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akizungumza na watoto wakati
alipotembelea bwalo la chakula la Shule ya Awali na Msingi ya Wonder
Kids ya mjini Ruangwa katika mahafali ya shule hiyo, Desemba 2, 2017.
Mke
wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akizungumza na watoto wakati
alipotembelea Bwalo la chakula la Shule ya Awali na Msingi ya Wonder
Kids ya mjini Ruangwa katika mahafali ya shule hiyo, Desemba 2,
2017.Kulia kwake ni binti yake, Zuleikha Kassim Majaliwa. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Watoto
wa Shule ya Msingi na Awali ya Wonder Kids wakiimba wimbo wa Shule yao
katika Mahafali ya Kwanza ya Shule hiyo iliyopo Ruangwa Mjini Desemba 2,
2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Wahitimu
wa wa Shule ya Msingi na Awali ya Wonder Kids wakicheza ngoma ya asili
katika Mahafali ya Kwanza ya Shulel hiyo iliyopo Ruangwa Mjini Desemba
2, 2017.
Mgeni
Rasmi katika Mahafali ya kwanza ya Shule ya Awali na Msingi ya Wonder
Kids ya mjini Ruangwa , Bw. Craig Ferla ambaye pia ni Mkurugenzi Mkazi
wa Taasisi ya Children in Crossfire akimkabidhi cheti kwa mhitimu wa
Mafunzo ya Awali katika shule hiyo, Jasmine Madamba, Desemba 2,
2017.Wapili kuil ni Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa
Baadhi
ya wazazi na waalikwa wa Mahafali ya Kwanza ya Shule ya Awali na Msingi
ya Wonder Kids ya Mjini Ruangwa wakimsikiliza Mke wa Waziri Mkuu, Mama
Mary Majaliwa wakati alipozungumza katika Mahafali hayo Desemba 2, 2017.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
MKE wa
Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa amewaomba wazazi wa wilaya ya Ruangwa
mkoani Lindi wahakikishe wanatumia sehemu ya kipato chao katika kuwekeza
kwenye elimu ya watoto wao.
Amesema
elimu ndiyo jambo pekee linaoweza kumsaidia mtoto katika kutimiza ndoto
zake za maisha pamoja na kumtoa katika kundi la wategemezi.Mama
Mary aliyasema hayo jana (Jumamosi, Desemba 2, 2017), katika maafali ya
shule ya awali na msingi ya Wonder Kids, iliyopo wilayani Ruangwa,
Lindi.Mke
wa Waziri Mkuu alialikwa katika maafali hayo kama mdau wa elimu.
Maafali hayo yaliyohusisha watoto wa awali ambao wanaingia darasa la
kwanza.
“Walimu
wanafanya kazi kubwa ya kuhakikisha wanafunzi hao wanajua kusoma
vizuri, hivyo wazazi watumie kipato chao kuwekeza katika elimu kwani
faida watakuja kuiona baadaye.”Alisema
kitaaluma yeye ni mwalimu hivyo anatambua kuwa walimu wanafanya kazi
kubwa ya kuhakikisha wanafunzi hao wanajua kusoma vizuri na wanakuwa na
tabia nzuri, hivyo wazazi hawana budi kushirikiana nao.
Pia
Mama Mary alitumia fursa hiyo kuwaomba wazazi wawatie moyo walimu kwa
sababu kazi wanayoifanya ni kubwa. “Wote ni mashahidi watoto wetu
tulivyowaleta na sasa ni tofauti.”Alisema
ni vizuri wazazi wakashiriki kikamilifu katika suala la elimu kwa
watoto wao ikiwa ni pamoja na kufuatilia maendeleo ya masomo yao badala
ya kuwaachia walimu peke yao.
Kwa
upande wake ,mgeni rasmi katika maafali hayo ambaye ni Muwakilishi Mkazi
wa Children in Crossifire Bw Craig Ferla aliwapongeza wanafunzi hao kwa
kutimiza moja ya hatua katika safari yao ya elimu na aliwasihi
waendele kupenda kwenda shule na kusoma kwa bidii.
Pia
aliwapongeza wazazi kwa kutambua umuhimu wa elimu ya awali na kuwapeleka
watoto wao kwenye shule hiyo ya Wonder Kids. “Wonder Kids ni mahali
sahihi ambapo mtoto anapata elimu na malezi bora.Alisema
elimu ya awali ninzuri kwa mtoto kwa kuwa inawawezesha kujua kusoma,
kuandika na kuhesabu, hivyo aliwaeleza Wanaruangwa kutumia vizuri fursa
ya uwepo wa shule hiyo katika wilaya yao.
Naye
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Bibi Nancy Tausi alisema Wonder Kid
ilianzishwa Januari, 2017 ikiwa na wanafunzi 117 ambao ni wa kuanzia
darasa la awali hadi darasa la tatu.Alisema
lengo la kuanzisha shule hiyo ni kuhakikisha watoto wanapata kujua
kusoma vizuri na kwamba wanatarajia kuanzisha darasa la kompyuta kwa
ajili ya watoto kujifunza TEHAMA pamoja na kuanza kufundisha lugha ya
Kifaransa.
EmoticonEmoticon