Judith Ferdinand, Mwanza
Timu ya Sandvik Fc imetoa kichapo cha goli 4-3 dhidi ya
wapinzani wao Mantrac Tanzania za jijini Mwanza katika mchezo wa
kirafiki uliotimua vumbi katika uwanja wa Nyamagana.
Mchezo huo ulioandaliwa na kampuni ya Sandvik Mining and
Construction (T) LTD ambao waliwakaribisha wenzao wa Mantrac Tanzania,
kwa ajili ya kuungana na watanzania na dunia kwa ujumla katika
kuadhimisha siku ya Ukimwi duniani inayofanyika kila mwaka Disemba Mosi.
Sandvik FC ilifunga magoli kupitia washambuliaji wake Petro
Ng’ oko dakika ya 13, Samwel Manga dakika ya 48 na Hamis Luhenga
dakika ya 60 na 72, huku Mantrac ifunga kupitia Emmanuel Joel dakika ya
10, na Hamfrey Kirutu dakika 30 na 52.
Akizungumza na BMG, Afisa Rasirimali Watu (HR) wa Sandvik
Mining and Construction (T), Deogratias Sendama ambaye ni Nahodha
Msaidizi wa timu hiyo,alisema, mchezo huo ni kwa ajili ya kuungana na
watanzani na dunia katika kuadhimisha siku ya ukimwi dunia, pia ulikua
mzuri na amefurahi kuwafunga wapinzani wao na hatimaye kuibuka na
ushindi.
Sendama alisema wataendelea kufanya mazoezi ili kuimarisha
kikosi zaidi, kwani mchezo ni afya na husaidia kuimarisha mahusiano kama
walivyofanya wao.
Pia aliwaomba, wafanyakazi wajitokeze kushiriki katika
michezo na mazoezi,ili kuimarisha afya na kuepusha mwili kuwa dhaifu
pamoja na kuondokana na msongo wa mawazo.
Kwa upande wake nahodha wa timu ya Mantrac Tanzania
Emmanuel Joel alisema, mchezo ulikua mzuri na walicheza vizuri japo kuna
makosa ya kibinadamu,hivyo wanajipanga kwa kufanya mazoezi ili katika
mechi nyingine waweze kufanya vizuri kwani hii walishtukizwa.
EmoticonEmoticon