Binagi Media Group
Watoto
wafanyakazi wa nyumbani kutoka Kata za Jiji la Mwanza ambao wamekuwa wakipatiwa
mafunzo ya utambuzi na Shirika la WOTESAWA, jana wameunda uongozi kwa ajili ya
kutetea haki na maslahi ya watoto wenzao.
Viongozi hao
kutoka kila Kata watakuwa na jukumu la kutoa elimu ya kupambana na ukatili
dhidi ya watoto wafanyakazi wa nyumbani ikiwemo wa ukatili wa kingono, kipigo
na utumikishwaji pamoja na kutoa taarifa katika ngazi husika pindi wanapobaini
mwenzao kakumbana na ukatili.
“Hakikisheni
mnakuwa sauti ya wenzenu, mnakuwa sauti za watoto wenzenu ambao wamefungiwa
kwenye mageti na hawana sauti. Mkiona mtoto mdogo ananyanyaswa hakikisheni
mnatoa taarifa ngazi mbalimbali ikiwemo shirika la WoteSawa ama kwa viongozi wa
serikali za Mitaa”. Alisisitiza Angel Benedicto ambaye ni Mkurugenzi wa
WOTESAWA, Shirika la Kutetea Haki za Watoto Wafanyakazi wa Nyumbani.
Viongozi
waliochaguliwa waliahidi kufichua vitendo vya ukatili katika jamii na kwamba
watatumia vyema fursa waliyoipata kusambaza elimu waliyoipata kwa waajiri wao
pamoja na watoto wafanyakazi wenzao katika mitaa yao ili kutokomeza ukatili
katika jamii.
Viongozi hao
walitoka Kata mbalimbali Jijini Mwanza ikiwemo Mkuyuni, Isamilo, Capripoint, Kirumba,
Pasiansi, Butimba, Igogo, Buhongwa na Mkolani ambapo pia watakuwa ni
wawakilishi wa watoto wafanyakazi wa nyumbani katika shughuli mbalimbali nchini.
Mkurugenzi wa WOTESAWA, Angel Benedicto akizungumza kwenye semina hiyo jana
Mkurugenzi wa WOTESAWA, Angel Benedicto
Viongozi wawakilishi wa watoto wafanyakazi wa nyumbani kutoka Kata mbalimbali Jijini Mwanza wakimsikiliza Mkurugenzi wa WOTESAWA, Angel Benedicto
Viongozi wa serikali za mitaa Jijini Mwanza ambao ni marafiki wa watoto wafanyakazi wa nyumbani Jijini Mwanza wakiwa kwenye semina hiyo
Bonyeza HAPA kusoma zaidi
EmoticonEmoticon