Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla mapema leo Oktoba
21,2017 amewasili Makao Makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii Mjini
Dodoma na kufanya mkutano na watumishi pamoja na wakuu wa taasisi ya
Wizara hiyo.
Awali
akiwasili Wizarani hapo, Waziri Dk. Kigwangalla alipata kupokelewa na
viongozi wakuu wa Wizara akiwemo Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja
Generali Gaudence Milanzi, Naibu Katibu Mkuu Aloyce Nzuki pamoja na
Naibu Waziri Japhet Hasunga (MB) na kisha kutembezwa kwenye ofisi
mbalimbali za wizara hiyo.
Akiwa
katika ukumbi wa mikutano wa Wizara hiyo, Waziri Dkt. Kigwangalla
aliwataka watumishi wote kuzingatia miiko ya kazi kwa kila mmoja
kusimama kwenye nafasi yake kama mtumishi aliyehaminiwa na Serikali.
“Kwa
pamoja tushirikiane kuijenga Wizara hii kama dhamana tuliopewa na Mh.
Rais wetu. Sisi tumekuja hapa kusimamia yale yote ya dhana na malengo
kusogeza mbele gurudumu la wizara hii.
Tunahitaji
sana uzoefu wenu, ufanisi wenu kwani mutaongeza spidi kwa kila mmoja
wenu..aliyekuwa anakamata majangili 5, aongeze juhudi akamate 10 ama
zaidi,
Aliyekuwa
analeta watalii wachache aongeze bidii alete wengi zaidi na wengine
hivyohivyo” Dkt. Kigwangalla alisema wakati akiteta na watumishi hao.
Pia
aliwataka wataalam wote kuzingatia ufanisi wao wa kazi awe Daktari,
Profesa ama mzoefu wa muda mrefu basi anahakika watamsaidia katika
kuinua Wizara hiyo.
Kwa
upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Generali. Gaudence Milanzi
amemwakikishia Waziri Dkt. Kigwangalla ushirikiano mkubwa katika kazi.
Aidha,
Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo na Wakuu wa Idara wa
Wizara hiyo wamepata kuwasilisha mada mbalimbali za idara zao na namna
ya utekelezaji majukumu yao.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangwalla akikaribishwa wizani hapo
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangwalla akisaini kitabu cha wageni alipowasili ofisini hapo.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akisaini kitabu cha
wageni wageni kwa Ofisi ya Waziri wa Wizara hiyo katika Makao makuu ya
Wizara ya Maliasili na Utalii eneo la Kilimani Barabara ya askari mjini
Dodoma. kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,
Dkt.Aloyce Nzuki.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maliasili na utalii, Mej. Jen. Gaudence Milanzi
akizungumza na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangwalla
wakati alipowasili ofisini hapo Makao makuu ya Wizara ya Maliasili na
Utalii eneo la Kilimani Barabara ya askari mjini Dodoma.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maliasili na utalii, Mej. Jen. Gaudence Milanzi
akimtembeza kwenye viunga vya Wizara hiyo Waziri wa Maliasili na Utalii,
Dkt. Hamisi Kigwangwalla. Wengine watendaji wakuu wa wizara.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangwalla akiwa na Naibu Waziri
wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga wakiteta jambo baada ya
kuzungumza na Watumishi katika Makao makuu ya Wizara ya Maliasili na
Utalii eneo la Kilimani Barabara ya askari mjini Dodoma.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maliasili na utalii, Mej. Jen. Gaudence Milanzi
akimkaribisha Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangwalla
katika mkutano huo.
Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini cha Wizara ya Maliasili na
Utalii, Dorina Makaya akitoa neno la shukrani mara baada ya Waziri wa
Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangwalla kumaliza kuzungumza na
Watumishi wa makao Makuu mjini Dodoma.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangwalla ( katikati )
akizungumza na Watumishi na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya
Maliasili na Utalii mara baada kuwasili kwa mara kwanza katika Makao
makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii eneo la Kilimani Barabara ya
askari mjini Dodoma.
EmoticonEmoticon