Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza na wananchi wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Ofisi za serikali za kijiji cha Mtavira.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza na wananchi wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Ofisi za serikali za kijiji cha Mtavira.
Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Mtavira, Makilawa na Mteva wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Ofisi za serikali za kijiji cha Mtavira.
Mwenyekiti wa Kijiji Cha
Mtavira aliyejiuzuru Ndg Jilala Lutelemula akizungumza mbele ya wananchi wakati wa Mkutano wa hadhara kabla ya kujiuzuru.
Mkazi wa Kijiji cha Mtavira Wilayani Ikungi Ndg Nchambi Kadawi akieleza changamoto inayowakabili wakati wa mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu.
Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Mtavira, Makilawa na Mteva wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Ofisi za serikali za kijiji cha Mtavira.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza na wananchi wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Ofisi za serikali za kijiji cha Mtavira.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza na wananchi wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Ofisi za serikali za kijiji cha Mtavira.
Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Mtavira, Makilawa na Mteva wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Ofisi za serikali za kijiji cha Mtavira.
Na
Mathias Canal, Singida
Mwenyekiti wa Kitongoji Cha Kazizi Ndg Kurwa Maduka
amevuliwa uongozini na Wananchi Wakati wa Mkutano wa hadhara kutokana na tuhuma
za kuruhusu na kuingiza wavamizi katika hifadhi ya msitu zinazomkabili huku
wananchi hao wakipendekeza Aliyekuwa Kaimu Mwenyekiti wa Kitongoji hicho Ndg
Mussa Mkumbo kuendelea Kuhudumu katika nafasi hiyo.
Mkutano huo uliofanyika katika eneo la Ofisi ya
Kijiji Cha Mtavira na kuhudhuriwa na wananchi 353 kutoka Kijiji Cha Makilawa,
Mtavira na Mteva Kata ya Makilawa umepelekea pia Mwenyekiti wa Kijiji Cha
Mtavira Ndg Jilala Lutelemula kujiuzulu kutokana na tuhuma mbalimbali
zinazomkabili ikiwemo tuhuma za kuchukua Rushwa ili kuwaacha wafugaji waendelee
kuishi na kuharibu msitu.
Mara Baada ya Mwenyekiti huyo kujiuzulu katika
Mkutano huo Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu Aliagiza
kuitishwa Mkutano wa wananchi haraka iwezekanavyo ili kuchagua Mwenyekiti mpya
ambapo pia ameagiza Mwenyekiti huyo kutiwa nguvuni ili kulisaidia Jeshi la
polisi kubaini wahujumu wa msitu huo.
Mhe Mtaturu pia aliliamuru Jeshi la polisi kumtafuta
popote alipo aliyekuwa Mwenyekiti wa Kitongoji Cha Kazizi Ndg Kurwa Maduka
kutokana na tuhuma zinazomkabili ikiwemo kuzuia wananchi kuhama katika msitu
huo Jambo ambalo Ni kosa kisheria.
Usiku wa kuamkia Octoba 17, 2017 Mhe Mtaturu
aliongoza Kamati ya ulinzi na usalama Wilaya ya Ikungi kuwasaka na kuwakamata
wavamizi wa msitu wa Minyughe wanaoendesha shughuli za kibinadamu ikiwemo
Makazi, kilimo na Ufugaji kinyume na Tangazo la serikali (GN) ya kuanzisha
hifadhi ya msitu wa Minyughe ya Mwaka 2007.
Katika Oparesheni hiyo Kamati ya ulinzi na usalama
pamoja na mambo mengine pia iliyobaini ukiukwaji wa taratibu unaofanywa na
baadhi ya viongozi wa Vijiji na Vitongoji ikiwemo kuwauzia mavamizi maeneo kwa
kutoa Rushwa ya fedha au Mifugo.
Mhe Mtaturu ameiagiza Taasisi ya kupambana na kuzuia
Rushwa (TAKUKURU) Kuwahoji wote wanaotuhumiwa katika sakata la kuruhusu
wavamizi wa hifadhi ya msitu.
Alisema kuwa Ni aibu kubwa kwa viongozi kujihusisha
na tuhuma mbalimbali zinazoichafua serikali, Kuvunja heshima na Uaminifu wa
wananchi kwa serikali yao.
"Dhambi ya viongozi kuwaacha kwa makusudi
wananchi waharibu misitu itaendelea kuwatafuna viongozi hao kwani wamewasababishia wananchi kuingia hasara ya kuchomewa nyumba zao ambazo
walidhani Ni makazi ya kudumu, Ni dhahiri kuwa hatuwezi kuvumilia Nchi ikawa
inaongozwa ovyo ovyo ilihali Kuna sheria, taratibu na kanuni" Alikaririwa
Mhe Mtaturu
Mhe Mtaturu pia alisema kuwa ili kunusuru misitu
kuharibiwa na wavamizi itaundwa Bodi ya
Misitu ambayo itashirikisha Wajumbe kutoka kila Kijiji katika Vijiji 24
vlivyopo katika Kata 8 zilizopitiwa na msitu huo wa hifadhi.
Pia aliwataka viongozi wa Vijiji, Kata na Kamati
zote za misitu kushirikiana kwa karibu na serikali ili kutunza misiti kwani
ndio Msingi wa uimarishaji wa Mazingira na uoto wa asili.
Mhe Mtaturu alisema kuwa dhamira ya kuhifadhi misitu
Ni kutunza Mazingira na uoto wa asili hivyo wananchi kufanya shughuli za
kibinadamu Ni kinyume na sheria ya misitu namba 14 ya mwaka 2002.
Sambamba na hayo pia Mhe Mtaturu aliwasihi wananchi
kuanza kuandaa mashamba kwani msimu wa Kilimo umekaribia huku akiwasisitiza
kuendelea kumuunga Mkono Rais wa Awamu ya Tano wa Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kutokana na kazi kubwa ya
kusimamia Rasilimali za Nchi anayoifanya.
Mhe Mtaturu alichangia shilingi milioni mbili kwa ajili ya ukarabati wa jengo litakalotumika kwa ajili ya kituo cha polisi cha muda huku Akielekeza wananchi, serikali ya kijiji na Kata kusaidia ukarabati wa kituo hicho sambamba na ujenzi wa kituo kipya cha Polisi cha Kata ya Makilawa.
Hifadhi ya msitu wa Minyughe ilianzishwa kwa Tangazo
la serikali (GN) Mwaka 2007 ina jumla ya hekta 264,600 ina manufaa makubwa
katika utunzaji wa mazingira na uoto wa asili kwa urahisi wa upatikanaji wa
mvua na urahisi katika uimarishaji wa sekta ya kilimo sambamba na ushoroba
(Njia ya Tembo).
EmoticonEmoticon